Mlolongo wa Kitume

Mlolongo wa Kitume (kwa Kiebrania האפיפיור הירושה, kwa Kigiriki Αποστολική διαδοχή) ni jambo linalodaiwa na imani ya baadhi ya madhehebu ya Ukristo, ya kwamba ni lazima viongozi wa Kanisa washiriki mamlaka ya Mitume wa Yesu katika mlolongo usiokatika wa kuwekewa mikono na maaskofu katika kuwapatia daraja takatifu.

Mlolongo wa Kitume unasadikiwa kupitia tendo la maaskofu kumwekea mtu mikono kichwani na kumuombea katika kumpatia daraja takatifu.

Imani hiyo inatiwa maanani hasa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, lakini pia Waanglikana na wengineo.

Kwao, maaskofu wa leo ni waandamizi wa wale wa jana na juzi hata kurudia kwa wale waliowekewa mikono na mitume wenyewe katika karne ya 1.

Mlolongo huo unahakikisha uhalali wa mamlaka yao katika kufundisha, kutakasa na kuongoza.

Kwa madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti, suala la mikono si la lazima, kwani kwao ni muhimu zaidi kuendeleza mafundisho ya mitume.

Vyanzo na viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mlolongo wa Kitume kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.