Mnara wa taa wa Port Said

Mnara wa taa nchini Misri

Mnara wa Taa wa Port Said ni mnara wa taa ambao ni moja kati ya alama muhimu za usanifu za utalii katika jiji la Port Said nchini Misri. Ikizingatiwa ni moja ya mfano wa kipekee wa uvumbuzi uliofanywa wakati wa karne ya 19 katika jiji hilo. Mnara wa taa uligunduliwa na François Coignet kutokana na mapendekezo ya utawala wa Khedive wa Misri na Isma'il Pasha wa Sudan. Ujenzi ulikamilishwa mnamo mwaka 1869, wiki moja kabla ya uzinduzi wa Mfereji wa Suez. Mnara huo wa taa ulijengwa ili kuongoza meli zinazopita kwenye mfereji huo. Mnara huo wa taa una umbo lenye pembe nane na urefu wa mita 56.

Historia hariri

Kuanzia mwaka 1868 hadi mwisho wa utawala wa Khedive Ismail aliamuru ujenzi wa minara ya taa sehemu tofauti tofauti kwenye pwani ya Mediterania ya Misri.[1] Mnara wa Port Said ulikua Miongoni mwa minara muhimu na maalum kwa sababu ya uhusiano wa kibiashara na Suez Canal.

Wakati huo, Mnara huo wa taa ulikua moja ya minara ya iliyo stahili sifa za kimataifa..[2][3][4]

Picha hariri

Viungo Vya Nje hariri

  • [1] (in English)
  • [2] (in English)

Marejeo hariri

  1. "Archived copy". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 April 2011. Iliwekwa mnamo 2011-02-07.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate= (help)
  2. Port-Saïd : architectures XIXe-XXe siècles. IFAO. 2005. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-26. Iliwekwa mnamo 2021-06-05.  Text "accessdat" ignored (help)
  3. Frost, G.H. (27 June 1885). Engineering News and American Contract Journal, Volumen 13. University of Iowa. uk. 406.  Text "accessdate" ignored (help); Check date values in: |date= (help)
  4. Port-Saïd : Architectures XIXe-XXe siècles Broché – 21 avril 2011
  Makala hii kuhusu maeneo ya Misri bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mnara wa taa wa Port Said kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.