Molière
Molière ilikuwa jina la kisanii la Jean-Baptiste Poquelin (15 Februari 1622 - 17 Februari 1673) aliyekuwa mwandishi mashuhuri nchini Ufaransa. Alikuwa maarufu kama mwigizaji na mwandishi wa tamthiliya.
Alizaliwa mjini Paris kama mtoto wa mfanyabiashara wa vitambaa. Mama alikufa mapema akalelewa na bibi yake akakaa muda mwingi kwenye shule ya Wajesuiti alipopata elimu nzuri. Pamoja na bibi yake alitembelea maigizo ya tamthiliya akawa mpenzi wa tamthiliya. Alipofikia umri wa miaka 21 alianzisha kampuni ya tamthiliya iliyoshindwa kiuchumi lakini akaendelea kuwa mwigizaji akazunguka kote Ufaransa akijulikana kwa jina la kisanii Moliere.
Tangu 1655 alitunga tamthiliya alizoonyesha na kundi lake la waigizaji. Mwaka 1658 mfalme kijana Louis XIV aliona maaigizo yake akampenda akamwita kuendelea kwenye makao makuu ya mfalme.
Katika miaka iliyofuata sifa za Moliere zikaongezeka; watu wengine hasa viongozi wa kanisa katoliki walichukia tamthiliya zake lakini mfalme alisimama upande wake na Moliere alizidi kufaulu na kuwa maarufu.
Kati ya tamthiliya maarufu ni "Tartuffe" inayosimulia habari za mnafiki wa kidini aliyejionyesha kama mcha Mungu lakini hali halisi alitafuta tu pesa akamdanganya mtajiri aliyemkubali kama mume kwa binti yake. Tamthiliya yake ya mwisho ilikuwa "Le Malade Imaginaire" (Mgonjwa kunyong'onyevu). Humo Moliere aliagiza mwenyewe akafa uwanjani wakati wa maonyesho ya nne ya tamthiliya hii.
Viungo vya Nje
hariri- Molière's works online Ilihifadhiwa 6 Septemba 2020 kwenye Wayback Machine. at toutmoliere.net (Kifaransa)
- Molière's works online at site-moliere.com
- Molière's works online at InLibroVeritas.net
- Molière's works online Ilihifadhiwa 14 Machi 2007 kwenye Wayback Machine. at classicistranieri.com
- Biography, Bibliography, Analysis, Plot overview Archived 2006-01-14 at Archive.today at biblioweb.org (in French)
- Moliere's Verses Plays Publication, Statistics, Words Research (in French)
- Professional quality parody - "The Life & Times of Moliere" at YouTube.com
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Molière kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |