Shirika la Yesu

(Elekezwa kutoka Wajesuiti)

Shirika la Yesu (kwa Kilatini Societas Iesu, kifupi S.J. au S.I. au SJ au SI) ni shirika kubwa la watawa wanaume 15,842 (2018) katika Kanisa Katoliki, lililoenea katika nchi 112 za kontinenti 6.

Ignas wa Loyola
Kanisa la Saint Pierre de Montmartre, Paris, (Ufaransa).
Mchoro wa ukutani wa Johann Christoph Handke kuhusu Papa Paulo III kupitisha sheria za shirika.

Wanashirika wanaitwa Wajesuiti na ni maarufu pia kwa elimu yao ya juu katika fani mbalimbali, za kidunia na za kidini.

Historia hariri

Mwanzilishi wake ni Ignas wa Loyola, Mhispania ambaye alikuwa mwanajeshi. Mwaka 1521 alijeruhiwa vibaya vitani. Alipokaa hospitalini muda mrefu akasikia wito wa Mungu uliobadilisha maisha yake. Kisha kuacha jeshi, akamtolea Bikira Maria upanga wake akawa "Mwanajeshi wa Kiroho". Alifuata kwa juhudi zote maisha ya kiroho na kutunga Mazoezi ya Kiroho ili kuongoza watu wamfuate Yesu Kristo.

Mwaka 1534, Ignas alikusanya vijana sita wakaweka nadhiri za ufukara, useja mtakatifu na utiifu, halafu ile ya kumtii daima Papa.

Kisha kusoma teolojia akapadrishwa. Akakusanya kikundi cha marafiki akiwaongoza kujenga maisha ya kiroho kwa njia ya mazoezi ya pekee. Wote walifuata utaratibu uleule. Kila mwaka walikutana kwa kipindi cha sala, kutafakari na kusoma kilichofuata hatua au mbinu maalumu. Wengi walianza kumfuata na chama chake kikakubaliwa na Papa mwaka 1540.

Shirika la Yesu lilikuwa chombo muhimu sana cha urekebisho wa Kikatoliki kikiwa jumuia ya mapadri iliyoongozwa na "Jenerali" wake akitumia nidhamu ya kijeshi.

Shabaha kuu ilikuwa kutetea Kanisa chini ya Papa.

Kila mwanachama alitakiwa kuwa na elimu ya juu. Hivyo Kanisa Katoliki liliimarika katika teolojia, jambo lililowahi kukazwa zaidi na Waprotestanti.

Mapadri Wajesuiti walifanya hasa kazi ya ualimu wakiunda shule na kufundisha vijana elimu pamoja na upendo kwa Kanisa Katoliki.

Mkazo mwingine ulikuwa kufufua utaratibu wa maungamo. Popote Ulaya Wajesuiti walikuwa washauri hasa wa watawala Wakatoliki. Waliposikiliza ungamo la dhambi zao walipata nafasi nzuri ya kuwapa mawazo na kusababisha hatua za serikali dhidi ya Waprotestanti.

Hivyo kwa athari ya Wajesuiti polepole Uprotestanti ulirudi nyuma katika nchi za Ulaya ambako wakazi wengi walikuwa wameanza kufuata mafundisho ya Martin Luther na Calvin lakini watawala walikuwa bado Wakatoliki.

Papa Fransisko ni wa kwanza kutokea shirika hilo.

Viungo vya nje hariri

Mafundisho ya Papa Benedikto XVI hariri

Hati za Wajesuiti hariri

Tovuti za Wajesuiti sehemu mbalimbali hariri

Afrika hariri

Amerika Kaskazini hariri

Amerika Kusini hariri

Asia-Oceania hariri

Ulaya hariri

Vyombo vya habari hariri

  Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shirika la Yesu kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.