Ndegejinga
Familia wa ndege wakubwa wa bahari
(Elekezwa kutoka Morus)
Ndegejinga | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 3:
|
Ndegejinga ni ndege wakubwa wa bahari wa familia Sulidae. Wana domo refu na mabawa marefu yaliyochongoka. Takriban spishi zote wana mwili mweupe na viasi mbalimbali vya nyeusi kwa mabawa na mkia. Spishi kadhaa zina namna kahawia na ndegejinga tumbo-jeupe ana rangi ya kahawa nzito na tumbo jeupe. Ndege hawa hupiga mbizi kutoka urefu mkubwa ili kukamata samaki au ngisi. Huzaa ndani ya makoloni makubwa. Jike hutaga yai moja au mayai mawili, lakini kinda atokaye kwanza katika yai lake amsukuma ndugu wake mdogo nje ya tundu. Huyu afa kwa njaa au aliwa na ndege wa aina nyingine.
Spishi za Afrika
hariri- Morus bassanus, Ndegejinga Kaskazi (Northern Gannet)
- Morus capensis, Ndegejinga Kusi (Cape Gannet)
- Sula dactylatra, Ndegejinga Kinyago (Masked Booby)
- Sula leucogaster, Ndegejinga Tumbo-jeupe (Brown Booby)
- Sula sula, Ndegejinga Miguu-myekundu (Red-footed Booby)
Spishi za mabara mengine
hariri- Morus serrator (Australasian Gannet)
- Papasula abbotti (Abbott’s Booby)
- Sula granti (Nazca Booby)
- Sula nebouxii (Blue-footed Booby)
- Sula variegata (Peruvian Booby)
Spishi za kabla ya historia
hariri- Sula humeralis (kati ya Pliocene)
- Sula sulita (Peru, mwisho wa Miocene)
- Sula magna (Peru, mwisho wa Miocene/mwanzo wa Pliocene)
Picha
hariri-
Ndegejinga kaskazi
-
Ndegejinga kusi
-
Koloni la ndegejinga kusi
-
Ndegejinga kinyago
-
Ndegejinga tumbo-jeupe
-
Ndegejinga miguu-myekundu na tumbo-jeupe
-
Ndegejinga miguu-myekundu
-
Australian gannet
-
Abbott's booby
-
Nazca booby
-
Blue-footed booby
-
Peruvian booby