Dante Terrell Smith (amezaliwa tar. 11 Desemba 1973) ni jina la kutaja mwigizaji na MC kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Mos Def na Yasiin Bey. Alianza kazi zake muziki wa hip hop akiwa na kundi la Urban Thermo Dynamics, ambamo aliweza kuonekana katika albamu za Da Bush Babees na De La Soul.

Mos Def
Mos Def at YBCA in San Francisco on 31 Desemba 2008
Mos Def at YBCA in San Francisco on 31 Desemba 2008
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Dante Terrell Smith
Amezaliwa 11 Desemba 1973 (1973-12-11) (umri 50)
Asili yake Brooklyn, New York, U.S.
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Rapper, mwigizaji, mwimbaji, mwanaharakati
Miaka ya kazi 1991 – hadi sasa
Studio Rawkus, Priority, Geffen, Downtown, GOOD Music, DD172
Ame/Wameshirikiana na Soulquarians, Black Star, Talib Kweli, Native Tongues Posse, Kanye West, Gorillaz, Massive Attack, Pharoahe Monch, Eminem, Blakroc, Robert Glasper Experiment, Mannie Fresh, Jay Electronica, Currensy, Dee-1

Akiwa na Talib Kweli, ameanza kundi la Black Star, kundi ambalo limetoa albamu ilkiyokwenda kwa jina la Black Star mnamo mwaka wa 1998. Alikuwa chachu kubwa wa hip hop chipukizi wa miaka mwishoni mwa miaka ya 1990 wakati yupo na studio ya Rawkus Records.

Akiwa kama msanii wa kujitegemea, amefanikiwa kutoa albamu kadhaa ambazo ni Black on Both Sides mnamo 1999, The New Danger mnamo 2004, True Magic mnamo 2006, na The Ecstatic iliyotoka mnamo mwaka wa 2009.[1]

Ijapokuwa awali alitambulika kwa kazi zake za muziki ambazo amezitoa, lakini tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000, kazi nyingi za Mos Def katika chideo zimemfanya awe rapa pekee aliyeweza vyema katika kazi zake za uigizaji. Anafahamika zaidi kwa kucheza kwake kama Brother Sam katika igizo la Kimarekani la Dexter. Mos Def amekuwa akijishughulisha mara kwa mara katika masuala ya kijamii na kisiasa.

Diskografia

hariri
Kolabo alizofanya

Marejeo

hariri
  1. [Mos Def katika Allmusic allmusic Biography]
  2. 2.0 2.1 "Mos Def & Talib Kweli to Reunite in 2012 for New Black Star Album". Complex. 2011-11-05. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-15. Iliwekwa mnamo 2012-04-17.

Viungo vya Nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:Mos Def Kigezo:Soulquarians Kigezo:GOOD Music