Kwa matumizi mengine ya jina moshi tazama makala ya maana moshi

[[Picha:

Moshi ya moto ya miti na matawi
Nigeria

Moshi kwa lugha ya kawaida ni wingu linalotokea pale ambako moto inawaka. Ni mchanganyiko wa vipande vidogo vya mata mango, matone ya kiowevu -hasa maji- na gesi mbalimbali pamoja na hewa. Mchanganyiko wa aina hii huitwa pia erosoli.

Matumizi ya moshi kwa kusudi

hariri

Mara nyingi moshi ni tokeo lisilotakiwa la moto lakini wakati mwingine inasababishwa kwa kusudi kwa matumizi ya kijeshi (wingo la kuficha jeshi), mawasiliano (alama za moshi), kidini (moshi ya uvumba), kuua wadudu (ufukizaji dhidi ya wadudu, panya n.k.), upishi (kuhifadhi samaki au nyama kwa kuikausha katika moshi inapopokea pia ladha inayotafutwa).

Moshi kama hatari ya afya

hariri

Moshi ya moto ni hatari ya afya. Wakati wa kuwaka moto ndani ya nyumba watu wanaweza kufa kutokana na gesi sumu katika moshi; hali halisi watu wengi wanakufa kutokana na moshi sumu kuliko na kuangamwa na moto yenyewe. Kuvuta moshi ndani ya mapafu kwa njia ya kupumua husababisha matatizo ya kiafya kuanzia mwako wa njia za pumzi hadi kansa na hii ni hatari ya kuvuta tumbako (kama sigara).

Sehemu za moshi

hariri

Sehemu za moshi na tabia yake hutegemea na fueli inayochomwa na mazingira ya moto.

Kama moto inaweza kutumia oksijeni nyingi inawaka kwa halijoto ya juu na hapo kiasi cha moshi kinapungua. Hapa vipande vidogo vya mata mango ni hasa majivu pamoja na mvuke wa maji. Moshi yenye mvuke wa maji huwa na rangi nyeupe-kijivu

Kama moto inapata oksijeni kidogo kiwango cha moshi huongezeka pamoja na gesi za sumu ndani yake kama vile monoksidi ya kaboni na mengine.

Pale ambako mafuta na plastiki vinachomwa rangi ya moshi huelekea kuwa nyeusi hasa kutokana masizi. Mafuta huchomwa sana ndani ya injini za mwako ndani kama injini za magari au majenereta na katika vituo vya umeme. Hapo ni muhimu kupunguza kiasi cha mosha kwa kutumia filta na mitambo ya kusafisha moshi