Mango ni moja kati ya hali maada. Maana yake ni imara, tofauti na kiowevu (majimaji) au gesi (kama hewa).

Katika hali mango atomu zinakaa mahali pamoja katika gimba hazichezi wala kutembea ndani yake. Kila atomu ina mahali pake. Gimba mango lina umbo, mjao na uzani maalumu. Umbo mango lina urefu, upana na kimo chake, tofauti na kiowevu kinachobadilisha umbo kufuatana na chombo chake au gesi isiyo na umbo wala mjao maalumu.

Kama mango inabadilika kuwa kiowevu tunasema inayeyuka. Kama inabadilika kuwa gesi au mvuke moja kwa moja tunaliita badiliko hili mvukemango.

Atomi katika hali maada mbalimbaliEdit

Tazama piaEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mango kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.