Fueli ni dutu inayowaka na kutoa nishati kwa njia inayoweza kutumiwa na binadamu. Mara nyingi fueli ni kitu kinachochomwa.

Ubao ulikuwa kati fueli za kwanza za binadamu

Kwa lugha ya kawaida si kila mara kikiwaka ya kwamba kinastahili kuitwa vile: ubao ukitumiwa jikoni kama kuni ni fueli; ubao ukiwaka hovyo wakati msitu inaharibika na moto si fueli.

Lakini kwa matumizi ya kitaalamu kile kinachowaka ni kampaundi za kaboni na hidrojeni ndani ya ubao na hii ni fueli yenyewe kwa maana ya kikemia.

Historia hariri

Kati ya fueli za kwanza za historia ni ubao inayotumiwa kama kuni. Baadaye watu waligundua njia ya kubadilisha kuni kuwa makaa ya ubao inayotunza nishati ndani ya kuni lakini ni nyepesi na kuchukua nafasi ndogo.

Baadaye watu waligundua ya kwamba mafuta mbalimbali ama kutokana na wanyama au mimea inaweza pia kuchomwa kupata nuru na joto kwa upishi.

Katika nchi kadhaa ambako mafuta ya petroli inafikia uso wa ardhi ilitumiwa katika hali ya kiasili na kuchomwa.

Baadaye watu waliona faida ya makaa mawe wakaanza kuichimba na kuchoma. Tangu karne ya 20 matumizi ya madawa kutokana na petroliamu yalisambaa kabisa kama vile petroli, diseli na mafuta ya taa.

Mara nyingi nishati ya fueli hutumiwa moja kwa moja kwa mfano kwa njia ya kuweka sufuria juu ya kuni, makaa au gesi inayowaka. Teknolojia ya umeme inawezesha watu kubadilisha nishati ndani ya fueli katika umbo tofauti ya nishati inayoweza kupelekwa kote kupitia nyaya za umeme. Asili ya umeme mara nyingi ni kuchomwa kwa fueli pia; kwa mfano katika vituo vya umeme mafuta ya petroli, dieseli au makaa mawe huchomwa kusudi la kuchemsha maji na mvuke wa maji unazungusha rafadha inayoteneneza umeme.

Aina za fueli hariri

Fueli yote hukusanya ndani yake nishati ya jua.

Fueli kisukuku hariri

Fueli nyingi inayotumiwa tangu karne ya 20 ni kisukuku. Hii ni hasa mabaki ya mimea ya milenia iliyopita iliyogeukia kuwa mafuta ya petroli au makaa. Fueli ya aina hii ina nishati kubwa kuliko kuni kwa sababu mabaki ya viumbe vya kale vilisukumwa kwa muda wa miaka mamilioni kwenye nafasi ndogo sana.

Fueli kisukuku imetambuliwa uchangia kwa kuongezeka kwa halijoto duniani. Sababu yake ni ya kwamba visukuku vinatunza kaboni daioksidi iliyokusanywa na mimea ya kale kwa muda wa miaka mamilioni. Tangu karne ya 19 wanadamu walianza kuchoma fueli hizi kwa wingi na kurudisha kaboni daioksidi yote ilyofunikwa kwa mika mamilioni hewani katika muda mfupi wa karne 1 au 2.

Fueli za kisukuku ni hasa

Fueli mbadala hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fueli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.