Mr Puaz

Meneja Wa Talanta Tanzania

Joel Vicent Joseph ( Anajulikana kama Mr Puaz[1]; alizaliwa Arusha, Tanzania, tarehe 31 Machi, 1985[2]) ni Meneja wa talanta[3][4], kutoka Tanzania. Mr Puaz alisainiwa chini ya studio ya rekodi iitwayo WCB Wasafi ili kumsimamia Harmonize.[5][6][7].

Mr Puaz
Mrpuaz.jpg
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Joel Vicent Joseph
Amezaliwa 31 Machi 1985 (1985-03-31) (umri 35)
Aina ya muziki Bongo Flava
Kazi yake Meneja Wa Talanta
Miaka ya kazi 2002 mpaka Sasa
Tovuti http://www.instagram.com/Mr_Puaz

Maisha ya awali na elimuEdit

Joel amezaliwa jijini Arusha, Tanzania tarehe 31 Machi 1985, mahali wazazi wake wamekulia na kuishi. Alihitimu masomo yake ya sekondari mwaka 2005 Marangu Secondary School na kuingia chuo cha uhandisi wa kompyuta kiitwacho New Horizon institute na kupata shahada yake ya kompyuta. Baadae aliendeleza masomo yake kwa kuchuku kozi mbali mbali kwa kutumia elimu ya mtandaoni ( E- Learning ) na kujichukulia vyeti vya kozi mbali mbali ikiwemo Usimamizi wa Ajira kutoka Harvards Business Publishing.

Maisha ya KaziEdit

Licha ya kuajiriwa katika makampuni mbali mbali yakiwemo Vodacom Tanzania Limited, MIC Tanzania Limited, Spice VAS Africa, Joel amekuwa mjasiriamali katika mambo mbali mbali ikiwepo upigaji picha [2] katika matukio mbali mbali ya burudani.

UandishiEdit

Joel ameanza uandishi akiwa na umri wa miaka 26, na hii ilitokana na kumiliki baadhi ya blogu zinazotoa makala mbali mbali za burudani, Amekuwa pia akiandika makala mbali kupitia media kubwa duniani kama Thrive Global, Tech Crates , Allbusiness na Marketing Insiders[8].

Maisha ya KimuzikiEdit

Mr Puaz[9] alianza muziki akiwa na miaka 21, Alikuwa akijihusisha na kuimba nyimbo za wasanii wengine (Cover Songs) ambapo ilimpelekea kujua kwamba ana uwezo wa kuimba hivyo kutunga nyimbo zake mwenyewe. Mwaka 2005 Mr Puaz aliingia kurekodi wimbo wake wa kwanza uitwao "SWEET BABY " iliyorekodiwa chini ya studio za Grandmaster Records zilizopo jijini Arusha,Tanzania.2006 alishiriki kutoa wimbo mwingine akiwa katika kundi akitumia jina Nizzo B[10]. Wimbo huo unaitwa "USIKU WA LEO" kazi ambayo imefanya vizuri kwenye Purebreak chart kubwa za Ufaransa.

Kazi yake ya meneja wa talantaEdit

Mnamo mwaka 2018 Mr Puaz[11] alisainiwa chini ya usimamizi wa studio rekodi iitwayo WCB Wasafi kwa ajili ya kumsimamia mwanamuziki Harmonize katika kazi zake. Moja kati ya mafanikio ya kazi kubwa alizofanya ni kujenga Harmonize na kuikuza sanaa yake ya muziki. katika kazi zilizoleta mafanikio makubwa moja wapo ilikuwa ni "kwangwaru" ambayo ni kazi ilibadilisha maisha ya mwanamuziki Harmonize kwa upande mkubwa , na hii ilimpa nafasi kubwa sana mr Puaz ya kuwa mmoja wa mameneja hodari wa Talanta Tanzania. kuacha "kwangwaru"" Mr Puaz amezisimamia kazi nyingine zikiwemo " Dm Chick" iliyomshirikisha mwanamuziki waGhana " Sarkdie" , Atarudi pamoja na Kadamshi. " Kwangwaru iliwezakuchukua nafasi mbali mbali na kushiriki katika tuzo mbali mbali Afrika ikiwemo African Muzik Awards ( AFRIMMA ). Licha ya kuwafanya kazi na Harmonize , pia Mr Puaz ameshawahikufanya kazi na msanii Shetta akiwa kama meneja wake.[10] Mwaka 2018 mwishoni Mr puaz alitangaza rasmi kuacha kufanya kazi WCB Wasafi na kuacha kufanya kazi na msanii Harmonize.[12] Kwa mujibu wa BBC[3] ilieleza kuwa Mr puaz alitengana na mwanamuziki huyo kwa sababu ya kutofautiana katika mazingira ya kazi na vile vile kauli.

AlbamuEdit

Jina la wimbo Mwaka
"Sweet Baby" 2004
"Usiku wa leo" 2015

MarejeoEdit

 1. Mr Puaz (en). Music In Africa. Iliwekwa mnamo 2018-07-04.
 2. 2.0 2.1 http://www.tanzaniatoday.co.tz/news/get-to-know-more-about-the-multi-talented-mr-puaz
 3. 3.0 3.1 Hamornize atengana na meneja wake (in en-GB), 2019-01-03, retrieved 2019-01-21 
 4. Mr Puaz Biography, Songs & Albums (en). AMDb. Iliwekwa mnamo 2019-01-24.
 5. Meet the man tasked to handle Harmonize by Diamond (Photos) (en-US). Facebook (2018-05-08). Iliwekwa mnamo 2019-03-05.
 6. Watiri, Sue, Meet the man tasked to handle Harmonize by Diamond (Photos) (in en-US), retrieved 2018-07-04 
 7. "ONE ON ONE: Harmonize", Daily Nation (in en-UK), retrieved 2018-07-04 
 8. "Avoiding Ghost Followers on Instagram", Marketing Insiders (in en-US), retrieved 2018-07-04 
 9. Tanzanian singer 'to publish music business book' (en). Music In Africa (2018-08-09). Iliwekwa mnamo 2019-01-24.
 10. 10.0 10.1 Steve Biko (2019-02-09). Mr Puaz (en-US). Afro Muziki. Iliwekwa mnamo 2019-03-05.
 11. Mr Puaz Biography, Songs, Age, Lifestyle and family (en-US). Informationcradle (2019-02-08). Iliwekwa mnamo 2019-03-05.
 12. Queen Serem (2019-01-04). EXCLUSIVE: Harmonize's manager Mr Puaz exits WCB (en-GB). Mpasho News. Iliwekwa mnamo 2019-03-05.

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mr Puaz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.