Checklist inasaidia kukagua makala mpya.

1. Maudhui hariri

  • Je matini inaeleweka? Muundo wa sentensi ni Kiswahili? (kama mtungaji alitumia google translate, sentensi mara nyingi ni za ajabuAJABU)
  • Je maana ya makala inaeleweka (kama mtungaji alitafsiri sehemu ya kwanza ya makala ya enwiki pekee, wakati mwingine haieleweki kwa nini makala iwepo katika wikipedia)
  • Je tahajia ya maneno ni sawa?
  • Je makala inaonyesha marejeo na / au vyanzo vya habari? (enwiki si chanzo wala si marejeo)
  • Je makala ina marejeo hai? (wakati mwingine mhariri anaweka marejeo yaliyokwishakufa na hivyo kuacha alama nyekundu kwenye makala)
  • Je marejeo yamekaa sehemu sahihi? (kuna wakati mtu anaweka marejeo yasiyo sahihi katika sentensi kwenye makala, hasa wakati anapozungumzia takwimu)

2. Fomati hariri

  • Je (ma-)neno la kwanza kwenye makala ni sawa na lemma (=jina la makala) likionekana kwa herufi koze (bold)?
  • Je ameweka vichwa vidogo kama ==Marejeo==, ==Viungo vya Nje== na kadhalika?
  • Matini iliyosogezwa
Je kuna matini yanayoonekana hivi?
  • Hii ni kosa katika matini ya kawaida. Kila mstari mpya ubane kushoto, bila kuacha nafasi tupu mwanzoni. Tunaweza kutumia fomati hii tukiingiza maelezo maalum au nukuu ndani ya matini ya kawaida.
  • Je ametumia jamii chini ya makala? Mfano: [[Jamii:MADA123]] . Pia alitumia jamii za kutosha?

3. Interwiki mwisho hariri

Kama makala iliandaliwa katika nafasi ya mtumiaji, haiwezi kuwa na kiungo cha interwiki. Lakini baada ya kuihamisha katika nafasi kuu, tusisahau kuunganisha interwiki!