Msafiri ni jina la kutaja wimbo uliotungwa na kuimbwa na kundi zima la Kwanza Unit. Mashairi yake anazungumzia hali halisi ya maisha. Kutoka dhikini kwenda katika maisha ya kati. Kama jinsi ilivyo nyimbo za hip hop, humu maelezo ya harakati ni mwanzo mwisho. Vilevile walifanya remixi yake na Mzee King Kikii. Wimbo unatoka katika albamu yao ya mwisho ya Kwanzanians.

"Msafiri"
Wimbo wa Kwanza Unit
Umetolewa 1999-2000
Umerekodiwa 1998-1999
Aina ya wimbo Hip hop
Lugha Kiswahili
Urefu 4:12
Studio MJ Records
Mtunzi Kwanza Unit
Mtayarishaji Rhymson

Tazama pia hariri

Viungo vya Nje hariri