Mto Kent
.
Mto Kent ni mto mfupi katika kata ya Cumbria nchini Uingereza. Mto huu unaanza katika milima inayozunguka Kentmere, na hutiririka karibu km 32 (maili 20) katika kaskazini ya Morecambe Bay, baada ya kupita Kentmere, Staveley, Burneside, Kendal na Sedgwick. Kijiji cha Arnside huwa katika kinywa cha Kent .
Mito Mint, Sprint na Gowan hujiunga na Kent kaskazini ya Kendal, na pia mto huu unaungwa na mto Gilpin na Mto Winster ukielekea mdomo wake.
Karibu na chanzo cha mto huu ni hifadhi ya Kentmere, ambayo ilijengwa katikati ya miaka ya 1800 kudhibiti mtiririko wa mto huu, ambao wakati huo ulitumika katika viwaanda. Karibu na Sedgwick, mto huu hupitia katika korongo ya mwamba ambayo huwa na maporomoko ya maji kadhaa. Sehemu hii ni maarufu kwa Kayaka kwa kuwa na maji safi kwa siku kadhaa baada ya mvua.
Katika misimu ya mawimbi makubwa, bakuli ya mchanga inayojulikana kama Bore Arnside huundwa katika kinywa hiki kando na Arnside. Mawimbi haya huwa na urefu wa mita 0.5.
Mto huu ni eneo maalum la kuhufadhi hasa kutokana na idadi ya Crayfish wenye kucha nyeupe Pia ni eneo la uvuvi wa samaki. Katika Staveley kuna weir kubwa na nyingine iko katikati ya mji wa Kendal. Kuna makao ya samaki katika daraja la Barley katika Staveley. Mto huu mara nyingi ulitoa nguvu kwa viwanda vya kusaga katika historia yake, ikiwa ni pamoja na kinu ya Staveley bobbin na kinu cha maji cha Kentmere , na pia kiwanda cha karatasi cha James Cropper katika Burneside.
Tazama pia
hariri
54°15′N 2°47′W / 54.250°N 2.783°W
Makala hii kuhusu maeneo ya Uingereza bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Kent kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |