Mtolondo-misitu
Dume la Mtolondo-misitu Habeshi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Estrildidae (Ndege walio na mnasaba na mishigi)
Jenasi: Cryptospiza
Salvadori, 1884
Ngazi za chini

Spishi 4:

Mitolondo-misitu ni ndege wadogo wa jenasi Cryptospiza katika familia Estrildidae ambao wanatokea Afrika tu. Wanafana na mitolondo lakini ndege hawa ni wekundu juu na kijivu chini na kichwani. Hula mbegu hasa na wadudu pia, hususa makinda. Tago lao ni tufe la manyasi, nyuzinyuzi na vigoga lenye mwingilio kwa kando. Jike huyataga mayai 3-4.

Spishi

hariri