Mtomoko
(Annona cherimola)
Mtomoko
Mtomoko
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Magnoliids (Mimea ambayo maua yao yana mizingo ya tepali tatu na chavua yenye kitundu kimoja)
Oda: Magnoliales (Mimea kama mparachichi)
Familia: Annonaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mkonokono)
Jenasi: Annona
Spishi: A. cherimola
Mill.

Mtomoko (Annona cherimola) ni mti mdogo wa familia Annonaceae. Matunda yake yanayolika huitwa matomoko. Spishi hii huitwa mtopetope pia, lakini tafadhali jina hili litengee kwa Annona squamosa. Annona reticulata huitwa mtomoko pia, lakini mti huu ni nadra katika Afrika ya Mashariki. Mtomoko una maua madogo njanokijani yenye petali nene. Matunda yana umbo wa donge au moyo na rangi ya majani hadi kahawa yakiwa yaliyoiva. Nyama ni nyeupe yenye ladha tamu. Mbegu nyeusi ni kubwa kiasi.

Picha hariri