Kwanza: kuingia wakati Swala ya faradhi ina wakati ambao haiswihi kabla yake, wala baada yake isipokuwa kwa dharura. Asema Mwenyezi Mungu aliyetukuka: { Hakika Swala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalum} [4: 103],

yaani imefaradhiwa katika vipindi maalumu.

Nyakati za Swala ni: .

1. Wakati wa Alfajiri: Ni kuanzia kutoka alfajiri ya kweli, nao ni ule weupe unaokuwa kwenye pambizo upande wa Mashariki, mpaka kuchomoza jua.

2. Wakati wa Adhuhuri: Ni kuanzia kupinduka jua mpaka kivuli cha kitu kiwe mfano wake, baada ya kile kivuli cha kupinduka jua. Hivyo ni kwamba jua likichomoza kitu kinachosimama huwa na kivuli upande wa magharibi, kisha kivuli hiko huenda kikipungua kila jua likipanda mpaka kivuli kisimame. Kisha kivuli kinaanza kuongezeka, na ongezeko hili lianzapo hua ndio wakati wa kupinduka.