Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Pamoja na salamu asante kwa kutaja mada ya maana katika jaribio lako la kwanza lakini nilipaswa kuifuta. Maana wachangiaji wote hutakiwa A) kuangalia fomati yetu ya habari, B) kuheshimu mwiko ni marufuku kumwaga hapa maudhui kwa njia ya kopi-paste kutoka tovuti nyingine na C) kufuata msimamo wa kutopendelea upande. Ukiweza kueleza desturi au mafundisho ya dini fulani karibu lakini bila lugha ya ndani ya dini hili (jinsi matini yako inayotuia lugha ya kumsifu anayeaminiwa katika Uislamu; lugha hii hatupokei hapa kwa dini yoyote).Kipala (majadiliano) 16:18, 24 Februari 2020 (UTC)Reply

Maana ya saumu za sunna hariri

Umeleta mada hii; tena naona ni mada ya maana lakini umenakili matini yote kutoka sehemu nyingine ya intaneti. Ninakuta manen yaleyale hapa www.facebook.com › sw.islamkingdom, www.pinterest.es, www.al-feqh.com na www.kenyatalk.com. Kunakili na kubandika kwetu ni marufuku kabisa kwenye wikipedia. Umeelimishwa kuhusu kanuni hizi uliopewa maelezo ya juu kenye ukurasa huu. Nimeweka alama ya "FUTA" kwenye ukurasa. Una siku 5 kusahihisha makala, yaani kueleza mada kwa maneno yako mwenyewe. Menginevyo itafutwa. Tafadhali soma Wikipedia:Mwongozo! Kipala (majadiliano) 20:14, 10 Machi 2020 (UTC)Reply

Onyo hariri

Fatuma naona unajitahidi kuchangia lakini unarudia yaleyale maana kuleta matini unazonakili kutoka tovuti nyingine ambayo ni haramu kwenye wikipedia. Ninakubana sasa kwa siku tatu na kufuta makala yako. Kama utarudia yaleyale baadaye nitakubana kwa daima. Karibu kuuliza maswali.Kipala (majadiliano) 17:22, 20 Machi 2020 (UTC)Reply

Unabanwa kwa wiki 1 hariri

Unaendelea kunakili matini kutoka al-feq.com. Hapa ni marufuku kuleta matini na picha zilizonakiliwa kutoka tovuti nyingine. Umeshapata onyo lakini unaendela. Nimekuhurumia sasa, ukirudia utabanwa kabisa. Nakushauri kuwasiliana na sisi wasimamizi, unaweza kupata msaada wa kuhariri. Lakini usiendelee hivyo. Kipala (majadiliano) 11:10, 26 Machi 2020 (UTC)Reply

Tangazo hariri

Habari ndugu Mwanawikipedia!

Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA

Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo

Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuainisha vitu vya msingi vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) wa Wikipedia na pale wanawikipedia wanapowasiliana kwenye Wikipedia au ana kwa ana katika warsha na mikutano ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kukithiri kwa baadhi ya Wanawikimedia kukumbana kufanyiwa unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Hivyo, wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huo Hapana baada ya kuusoma mwongozo huo unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 15 April 2020.

Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia

Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Dar es Salaam ili tuweze kujadiliana na kubadilishana uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla na miradi waliyoitekeleza tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.

Ndimi AMtavangu (WMF) (majadiliano) 22:23, 5 Aprili 2020 (UTC)Reply

Kubanwa kwa miezi 3 hariri

Umerudia kuleta maudhui uliyonakili kutoka tovuti nyingine. Nahofia kwamba husomi ukurasa wako wa majadiliano. Labda unasoma lakini hujali. Basi ninafunga akaunti yako asa kwa miezi 3. Ukirudia baadaye, nitakufunga milele. Kipala (majadiliano) 12:03, 23 Aprili 2020 (UTC)Reply