Monica G. Turner hariri

Monica G. Turner ni mwanaikolojia wa Kimarekani anatambulika kutokana na kazi anayofanya katika Hifadhi ya Kitaifa ya Yellowstone tangu kulipotokea mioto ya mwituni mnamo 1988. Monica sasa ni Profesa wa Eugene P. Odum wa Ikolojia katika Chuo Kikuu cha Wisconsin–Madison. [1]

Maisha na kazi hariri

Mwanaikolojia huyu alilelewa katika vitongoji vya Long Island vipatikanavyo nje kidogo ya jiji la New York. Baba yake alikuwa wakili aliyejiajiri na mama yake alikuwa mtendaji wa shirika liitwalo Girl Scouts. Turner alihitimu na kupata stashahada yake katika Biolojia summa cum laude kutoka Chuo Kikuu cha Fordham mnamo 1980. Turner aliendelea kupokea stashahada ya udaktari (Ph.D.) ya Ikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Georgia.

Baada ya kumaliza elimu yake ya udaktari, alikaa katika Chuo Kikuu cha Georgia kama mhitimu wa udaktari anaefanya uchunguzi. Monica alifanya kazi na Eugene P. Odum kuchunguza mabadiliko katika matumizi ya ardhi katika ya mji wa Georgia, moja ya masomo ya awali ya ikolojia ya mazingira ya Marekani.

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtumiaji:Garnacite kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.