HISTORIA YA GERALD MOSES HYERA (GEROLD MOSES HYERA) (HYERA GERALD)

Gerald Moses Hyera alizaliwa Mwaka 1992 May 25, Katika wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma. Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Myanga yanga iliyoko wilayani humo kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2006, Baada ya kuhitimu alijiunga na shule ya sekondari ya Kindimba wilayani humo humo mwaka 2007 na kuhitimu mwaka 2010.

Baada ya kuhitimu alijiunga na shule ya sekondari ya upili kidato cha 5&6 wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma katika shule ya sekondari ya Jeshi inayoitwa Ruhuwiko mwaka 2011 na kuhitimu 2013, Baada ya kuhitimu alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa -JKT katika 832 KJ Ruvu,Mujibu wa sheria kwa kipindi cha miezi mitatu na baadae kuhitimu Mafunzo.

Baada ya kuhitimu alijiunga na Chuo kikuu Cha Tumaini Makumira Tawi la Mbeya ambapo alisoma Degree yake ya Kwanza ya Sanaa na elimu (Bachelor degree of Arts with education) kuanzia mwaka 2013 October na kuhitimu 2016 July.


Baada ya kuhitimu alijikita katika uandishi wa kazi za kifasihi na baadae mwaka 2017 alijiunga na Kampuni ya bima ya Bumaco (Bumaco insurance Company) akifanya kazi kama Afisa wa bima hadi mwaka 2019.

Mwaka huo 2019 July alijiunga na Jeshi la kujenga Taifa kwa kujitolea na kupata mafunzo ya kijeshi ambapo alitumikia jeshi hilo na kuhitimu October 2022. Na baada ya kuhitimu ameendelea na majukumu yake katika harakati za kutafuta Maisha