Maria Alphonce, na mkuu wa shule (SJMC) baada ya kukabidhiwa rasmi zawadi kutoka Wikipedia
Lugha
sw Mtumiaji huyu ni mwongeaji wa Kiswahili Fasaha.
en-2 This user is able to contribute with an intermediate level of English.


KWC Mtumiaji huyu ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
KWC Mtumiaji huyu ni mshiriki katika Shindano la Wikipedia ya Kiswahili la 2009.   (Submissions)


Ninaitwa Maria Alphonce. Ni Mwafrika ninayeishi Tanzania. Ninasoma masuala ya Mahusiano ya Umma na Matangazo katika Shule ya Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Ummna (SJMC) Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. Nimejiunga katika Wikipedia kwani ninapenda kuandika makala hususani ya Kiswahili na pia ni baada ya kuona tangazo kuhusu ya mashindano haya ya kuandika makala katika wavuti wa Wikipedia.

Nasikia furaha sana kuwa mmoja kati ya washiriki katika mashindano haya na ni matumaini yangu kuwa nitafanya vizuri na kuweza kuikuza lugha yetu ya Kiswahili.

Nasikia furaha zaidi kwa kuweza kuwa moja kati ya washindi wa kundi la kwanza, katika shindano hili la Wikipedia, nahisi furaha kwa kupata zawadi nzuri lakini nahisi fahari zaidi kwa kuweza kuongeza hazina ya makala katika lugha ya Kiswahili, makala ambazo zitaweza kusomwa ulimwengu mzima. Shukrani zangu za dhati kwa wote walionisaidia kupata ushindi huu.

Nilifurahi kuwa moja ya washindi katika shindano la Wikipedia, najitahidi kuendelea kuandika makala ya kiswahili.