Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

(Elekezwa kutoka University of Dar es Salaam)
Nembo ya chuo kikuu.
Ukumbi wa Nkrumah.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kifupisho chake UDSM kutoka Kiingereza "University of Dar es Salaam") ni chuo kikuu cha kwanza nchini Tanzania[1]. Ni chuo cha umma kilichopo katika jiji la Dar es Salaam.

HistoriaEdit

Kilianza kuwa chuo kikuu mwaka wa 1970 baada ya kutengwa kwa Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki katika vyuo vikuu huru vitatu: Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda), Chuo Kikuu cha Nairobi (Kenya) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam[2].

Kabla ya hapo kilianzishwa mwaka 1961 na kushirikiana na chuo Kikuu cha Uingereza. Chuo kikuu kilijishirikisha na Vyuo vya Afrika Mashariki (UEA) mwaka 1963, muda mfupi baada ya Tanzania kuwa huru kutoka ufalme wa Uingereza.

Kiwango cha ElimuEdit

Mwaka wa 2019, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilitambuliwa kama chuo kikuu bora zaidi nchini Tanzania, hapo juu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo mjini Morogoro.[3] USDM kilitambuliwa kama chuo cha sitini na tisa kwa ubora zaidi wa elimu kwa Afrika.[4] Kinatambulika kama chuo cha 1885 kwa ubora wa kitaaluma duniani.[5]

TaalumaEdit

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinatoa programu kadhaa za shahada ya kwanza, kama vile: akiolojia, usanifu majengo, bayolojia, biashara, kemia, elimu ya mawasiliano, elimu ya komputa, masomo ya maendeleo, uchumi, elimu, uhandisi na elimu ya hali ya mazingira.[6] Chuo kinatoa programu kadhaa za shahada za Uzamili na Uzamivu, kama vile: elimu ya usimamizi wa fedha, sanaa, jiografia, sheria, isimu ya lugha, fasihi, uongozi, hisabati, utabibu, muziki, lishe, fizikia, sayansi ya mimea, elimu ya siasa, saikolojia, na sanaa za maonyesho.[7]

Maisha ya Chuo KikuuEdit

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kina maeneo matano mjini na karibu na mji wa Dar es Salaam. Mlimani iko kilomita kumi na tatu magharibi mwa jijini.[8] Chuo Kikuu ni nyumbani kwa wanafunzi 17,098 wa shahada ya kwanza, na wanafunzi 2,552 wa shahada za uzamili na uzamivu.[9]

Watu maarufu waliohitimu ChuoniEdit

Wahadhiri wanaofahamikaEdit

 • Molly Mahood, Profesa wa Kiingereza, 1954-1963
 • Walter Rodney, Mwanahistoria maarufu wa Guyanese, mwanaharakati wa kisiasa na msomi
 • Yashpal Tandon, Mtunga sera wa Uganda, mwanaharakati wa kisiasa, profesa, mwandishi na wasomi wa umma

TanbihiEdit

 1. Register of Universities (PDF). Tanzania Commission for Universities. Iliwekwa mnamo 15 July 2013.
 2. Welcome to the University of Dar es Salaam - Background. University of Dar es Salaam.
 3. URAP - University Ranking by Academic Performance. www.urapcenter.org. Iliwekwa mnamo 2019-07-28.
 4. URAP - University Ranking by Academic Performance. www.urapcenter.org. Iliwekwa mnamo 2019-07-28.
 5. URAP - University Ranking by Academic Performance. www.urapcenter.org. Iliwekwa mnamo 2019-07-28.
 6. University of Dar es Salaam-Programme. www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2019-07-28.
 7. University of Dar es Salaam-Programme. www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2019-07-28.
 8. "University of Dar es Salaam", Wikipedia (in English), 2019-07-20, retrieved 2019-07-28 
 9. "University of Dar es Salaam", Wikipedia (in English), 2019-07-20, retrieved 2019-07-28 

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.