Muziki wa Jibuti unashirikisha mitindo mbalimbali ambayo ni matokeo ya ushawishi mbalimbali ya kimuziki.

Kuhusu Jibuti hariri

Jibuti ni taifa dogo lipatikanalo katika Pembe ya Afrika ambayo imekuwa mitindo mingi ya muziki za humo nchini. Watu wa huko wamejikidhi kwa wengi katika mji wa uvuo ambao pia huitwa Mji wa Jibuti. Nchi hiyo imekuwa ikishirikishwa mataifa mengi, hivi maajuzi ikiwa Ufaransa. Jibuti ilikuwa nchi ya mwisho kupata uhuru kutoka Ufaransa.

Jibuti ina matabaka mawili: Kabila na Somali, pamoja na Wafaransa na Waarabu. Muziki wa Afra unafanana na Muziki wa Ethiopia ukiwa na ikiwa na vipengele vya Muziki wa Kiarabu. Historia ya muziki huu imenakiliwa katika ushairi na nyimbo za watu wake ambao ni wafugaji wa kuhamahama na inaanzia maelfu ya miaka iliyopita hadi wakati Jibuti ikifanya biashara za kubadilishana ngozi kwa manukato na Wamisri, Wahindi na Wachina. Ngano za Kisomali hujumuisha ushairi, na Methali, nyingi zao zikiwalenga mitume wa Sufi na maisha yao. Fasihi ya watu wa Afar imeundwa kimuziki na ni ya aina nyingi, ikijumisha nyimbo za Ndoa, Vita, kusifu na kujigamba.[1]

Wimbo wa Taifa hariri

Wimbo wa Taifa wa Jibuti ni Jibuti (Wimbo) ulioundwa mnamo 1977 huku maneno yake yakitoka kwa Aden Elmi na muziki ukitungwa na Abdi Robleh.[2].

Balwa hariri

‘’Miniature poetry’’ au “Ushairi Mdogo” uliovumbuliwa na mwendeshaji wa lori aliyekuwa akiitwa Abdi Deeqsi, unajulikana sana nchini Jibuti. Haya ni mashairi mafupi (balwo), sana sana yanayohusu mapenzi [1] “Balwo” pia ni mtindo wa muziki wa Somalia wa aina ya ‘’Pop’’.

Vyombo vya muziki hariri

Vyombo vya muziki vya Jibuti vinashirikisha tanbura, ambayo ni aina ya kijisahani [3]

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 Djibouti - Culture Overview. Expedition Earth. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-02-27. Iliwekwa mnamo 28 Septemba 2005. - Website no longer exists; link is to Internet Archive
  2. Djibouti. National Anthem Reference Page. Iliwekwa mnamo 28 Septemba 2005.
  3. Poché, Christian. "Tanbūra", The New Grove Dictionary of Music and Musicians, ed. S. Sadie and J. Tyrrell (London: Macmillan, 2001), xxv, pp. 62-63.
  Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Muziki wa Jibuti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.