Mwanasheria ni mtaalamu wa fani ya sheria. Mara nyingi huingia katika kazi ya wakili, lakini anaweza vilevile kufundisha sheria katika vyuo, kuwa mshauri wa kampuni n.k.

Ili kufahamu vizuri kuhusu kazi za mwanasheria ni vema ujiulize maswali haya, ‘Ni nini asili ya Sheria? Sheria inatoka wapi? au chanzo cha sheria ni nini?'

Kwa ufupi ni kwamba zipo dhana nyingi na tofautitofauti sana zinazoelezea asili ya sheria ambazo zimeelezewa na wasomi wa sheria wa karne zilizopita. Hata hivyo wasomi hawa wa sheria wanakubaliana kuwa asili ya sheria inaweza kufuatiliwa tangu kuanza kuishi kwa mwanadamu hapa ulimwenguni. Hivyo msimamo wa wasomi wa sheria wengi ni kuwa sheria ilianza pale watu walipoanza kuishi kama jamii.

Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanasheria kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.