Mwendomajisumaku
Mwendomajisumaku (Kiingereza: magnetohydrodynamics) ni maelezo ya giligili ziwezazo kupitisha umeme. Hasa inahusu mwenendo sumaku wa utegili au metali kiowevu zenye mabadiliko ya marudio madogo kwa kiwango kikubwa. Elimu hiyo hutumika sana katika uwanja nyingi kama fizikia ya dunia, fizikia ya jua, fizikia ya anga, na uhandisi.
Jina
haririJina mwendomajisumaku ni ambatani ya mwendo, maji, na sumaku. Jina katika Kiingereza, magnetohydrodynamics ni ambatani ya magneto- ("sumaku"), hydro- ("maji"), na dynamics ("mwendo" au "elimumwendo").
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwendomajisumaku kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |