Mwenge wa uhuru[1] (kwa Kiingereza Uhuru Torch) ni mojawapo ya alama za kitaifa za Tanzania [2].

mwenge wa uhuru katika stempu ya barua ya shilingi 20

Ina muundo wa tochi ya mafuta ya taa ambayo inaashiria uhuru na mwanga. Mwenge wa uhuru ulinyanyuliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro mnamo Desemba 9, 1961 na shujaa Brigedia Alexander Nyirenda Ilihifadhiwa 19 Mei 2023 kwenye Wayback Machine. ikiashiria kuangaza nchi na kuvuka mipaka kuleta matumaini palipo kukata tamaa, upendo palipo uadui na heshima palipo chuki. Sababu ya huyu brigedia kunyanyua mwenge huu ni kuonesha fahari ya nchi na pia kuleta matumaini kwa Watanzania wote kwa kutokata tamaa, kupendana, kuheshimiana na kutogombana ikimaanisha kuwa na ushirikiano.

Mbio za Mwenge wa Uhuru hufanyika kila mwaka kuanzia maeneo mbalimbali nchini.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Mwenge wa uhuru
  2. [https://www.bing.com/search?q=coat+of+arm+in+swahili&qs=n&form=QBRE&sp=-1&ghc=1&lq=0&pq=coat+of+arm+in+swahili&sc=10-22&sk=&cvid=C0CC9CAD9BCD4870ADA318A829D18AE6&ghsh=0&ghacc=0&ghpl=