Kilimanjaro (volkeno)

Milima ndani ya hifadhi ya Taifa ya KIlimanjaro nchini Tanzania
(Elekezwa kutoka Kilimanjaro (Volkeno))

Kilimanjaro ni jina la mlima mrefu kuliko yote barani Afrika. Mlima huo uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa mita 5,895 (futi 19,340).

Kilimanjaro mnamo 1911
Picha ya kwanza ya angani ya Kibo iliyochukuliwa na Walter Mittelholzer mnamo 1929
Tembo kwenye Hifadhi ya Kitaifa ya Amboseli dhidi ya Mlima Kilimanjaro
Mlima Kilimanjaro kama unavyoonekana kutoka manispaa ya Moshi katika Mkoa wa Kilimanjaro
mfano wa kilele cha mlima kilimanjaro
Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka Moshi
Kilele cha Kibo kwenye mlima Kilimanjaro

Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi ya mlima tu, ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hiyo mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja, hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima.

Kijiolojia Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko mnamo mwaka 1730.

Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru. Mtu wa kwanza kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kwa Kijerumani: Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.

Kibo ina theluji na barafuto ndogo kadhaa.

Jina

 
Ramani ya 1888 inayoonyesha jina "Kilima-Ndscharo" katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Asili ya jina "Kilimanjaro" haijulikani kikamilifu. Vyanzo vya kimaandishi vinajulikana tangu takriban mwaka 1860 ambapo wapelelezi Wazungu walitumia jina hilo katika taarifa zao wakidai "Kilimanjaro" ni jina la Kiswahili.[1] Pamoja na umbo hili kulikuwa pia na tahajia ya sehemu mbili ama "Kilima-Njaro"[2] au kwa namna ya Kijerumani “Kilima-Ndscharo”.

Johann Ludwig Krapf aliandika mnamo 1860 kuwa Waswahili kwenye pwani waliita mlima huo "Kilimanjaro". Alisema pia ya kwamba hao Waswahili walieleza maana yake kuwa ama “mlima mkubwa” au “mlima wa misafara” ingawa mwenyewe hakukubali maelezo hayo. Kwa elezo la mwisho "Kilima" kilimaanisha "mlima" na "Jaro" labda "misafara".[1]

Jim Thompson aliandika mnamo 1885 kuwa jina Kilima-Njaro lilichukuliwa mara nyingi kuwa na maana ya "mlima mkubwa" lakini mwenyewe alipendelea maelezo tofauti yaliyosema "mlima mweupe". [3] "Njaro" ni Kiswahili cha Zamani kwa "ng’ara".[4]

Vivyo hivyo Krapf aliandika ya kwamba aliwahi kuwatembela Wakamba mnamo 1849 walioita mlima “Kima jaJeu” yaani mlima mweupe [5] Leo hii Wakamba wangesema “Kiima Kyeu” na elezo hili limekubaliwa na watafiti mbalimbali.

Wengine huona ya kwamba ni Wazungu wasiojua Kiswahili vema waliochanganya “mlima” na “Kilima”.

Wengine wamejaribu kuona msingi wa jina katika lugha ya Kichagga. Hapo wanadai uwezekano kuwa "Kileman" limetokana na neno la Kichagga "kileme" linalomaanisha “kinachoshinda” au neno "kilelema" linalomaanisha "kilichokuwa vigumu, kilichoshindikana". Katika hoja hiyo "Jaro" imetokana na Kichagga “njaare” (aina ya ndege, au kufuatana na wengine chui) au kutoka neno “jyaro” (msafara). Elezo lingine ni kwamba Wachagga walisema mlima huo hauwezi kupandwa "kilemanjaare" au "kilemajyaro" na wapagazi au wafasiri kutoka pwani waliichukua kuwa jina la mlima na kutafsiri vile kwa Wazungu.

Tangu miaka ya 1880 mlima umekuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ukaitwa "Kilima-Ndscharo" kwa Kijerumani.[6]

Tarehe 6 Oktoba 1889 Hans Meyer alikuwa mtu wa kwanza anayejulikana kupanda mlima na kufika hadi kilele cha Kibo. Alichagua jina la "Kaiser-Wilhelm-Spitze" ("Ncha ya Kaisari Wilhelm"[7]).[8]

Jina hilo lilitumika hadi Tanzania ilipoundwa mwaka 1964,[9] na kilele kubadilishiwa jina kuwa "Uhuru", likiwa na maana ya "Kilele cha Uhuru" [10]

Jiolojia ya mlima na tabia za kijiografia

Kilimanjaro inapanda hadi mita 4877 juu ya tambarare karibu na mji wa Moshi uliopo miguuni pake. Hii inafanya kilele chake kuwa mita 5895 juu ya uwiano wa bahari.[11]

Kilimanjaro ni volkeno ya rusu iliyojengwa na rusu za majivu, zaha na mata nyingine. Ni volkeno ndefu kuliko zote duniani nje ya Amerika Kusini. [12]

Vilele vitatu vya kivolkeno juu ya Kilimanjaro ni

  • Kibo iliyo juu zaidi
  • Mawenzi yenye kimo cha mita 5149[13]
  • Shira yenye urefu wa mita 4005.[14] Vyote vitatu vina kasoko.

Mawenzi na Shira ni volkeno zimwe lakini Kibo ni volkeno iliyolala, ila inaweza kuwaka tena. [15]

Uhuru ni sehemu ya juu kwenye ukingo wa kasoko ya Kibo. Taasisi ya Tanzania National Parks Authority [16] na UNESCO zinataja kimo cha Uhuru Peak kuwa mita 5895. Kimo hicho kimetokana na upimaji uliofanyika wakati wa ukoloni wa Uingereza mwaka 1952. [17] Tangu upimaji ule kimo cha mlima kimepimwa tena: kinaonyesha kuwa mlima unapungua polepole. Kipimo kilikuwa mita 5892 mwaka 1999 na mita 5891 mwaka 2014.[17]

Muundo wa ndani wa Kilimanjaro haujulikani sana kwa sababu hadi sasa haujatokea mmomonyoko mkubwa unaoweza kufunua ndani yake.[18]

Shira

Kilele cha kale zaidi ni Shira iliyoanza kutema moto takriban miaka milioni 2.5 iliyopita ikaacha miaka milioni 1.9 iliyopita. Wakati ule upande wa kaskazini wa mzingo wa kasoko ulipinduka. [15] Leo hii Shira ina tambarare pana kwenye kilele chake kwenye kimo cha mita 3800; inawezekana hii kiasili ilikuwa kaldera iliyojaa lava. Mabaki ya mzingo wa kaldera yamepungua sana kutokana na mmomonyoko. Kabla ya kutoa moto na kutokea kwa mmomonyoko kimo cha Shira kilikuwa kati ya mita 4,900 na 5,200. Mata yake ni hasa lava pamoja na kiasi cha piroklasti. [15][18][19]

Mawenzi

Mawenzi na Kibo zilianza kulipuka (kutoa moto) takriban miaka milioni iliyopita.[15] Zimetengwa na tambarare ( "Saddle Plateau") kwenye kimo cha mita 4400.[20]: 3 

Miamba ya kijana kwenye Mawenzi ilitokea miaka 448,000 iliyopita. [15] Mawenzi huwa na mgongo wenye umbo la kiatu cha farasi mwenye ncha kali na kufunguka upande wa kaskazini-magharibi. Mgongo unakatwa na mabonde kadhaa na upande wa mashariki wa mlima umepungua kutokana na mmomonyoko. Mawenzi huwa na kilele cha pili kinachojulikana kwa jina la “Neumann Tower” chenye mita 4425.[15][18][19]

Kibo

Kibo ni pia ya kivolkeno yenye kimo kirefu ikiwa na upana wa kilomita 15 kwenye "Saddle Plateau". Ililipuka mara ya mwisho miaka 150,000 na 200,000 iliyopita na mlipuko huo ulifanya kasoko kwenye kilele cha Kibo cha sasa. Hadi leo gesi inatoka kwenye mashimo ardhini.[15][18][19] Kibo huwa na pia kwenye kilele chake chenye umbo kamili. Kuna kaldera yenye upana wa kilomita 2.5 na ndani yake pia iko kasoko ya Reusch. Jina hilo lilitolewa na serikali ya Tanganyika mwaka 1954 kwa heshima ya Mjerumani Gustav Otto Richard Reusch alipopanda mlima mara ya 25. [21][22] Ndani ya kasoko ya Reusch kuna shimo refu linalojulikana kwa jina la “ash pit” (shimo la majivu).[23] Wakati wa mlipuko wa mwisho uliotokea miaka 100,000 iliyopita sehemu za mzingo wa kasoko ziliporomoka na kuacha pengo kubwa. [24]

Kibo huwa na pia za kando zaidi ya 250 ambazo ni mashimo ambako gesi, zaha na piroklasti zilitoka kwenye pande za mlima wakati wa kuwa volkeno hai. Zilitokea miaka 150,000 hadi 200,000 iliyopita [15]. Zinapatikana hadi Ziwa Chala na Taveta upande wa kusini-mashariki na hadi Lengurumani upande wa kaskazini-magharibi. Zaha iliyotoka katika pia hizo za kando ilifunika sehemu kubwa ya pande za mlima.

Wamaasai wana kumbukumbu ya kuwa Ziwa Chala upande wa mashariki wa Kibo lilikuwa mahali pa kijiji kimoja kilichoharibika na mlipuko wa volkeno.

Maji yatoka mlimani kwa njia ya mito na vijito hasa upande wa kusini unaopokea mvua zaidi hasa juu ya mita 1200. Chini ya kimo hicho maji kwenye mito inapungua kutokana na mvukizo na matumizi ya binadamu. Mito ya Lumi na Pangani inabeba maji ya Kilimanjaro kuelekea mashariki na kusini. [25]

 
Mlima Kilimanjaro ukitokea kati ya mawingu.

Tabianchi

Tabianchi ya Kilimanjaro inaathiriwa na kimo cha mlima kinachoruhusu kufika kwa upepo kutoka bahari wenye unyevu mwingi na wakati mmoja pia upepo za juu sana. Tabia nyingine ni hali yake ya kuwa mlima wa juu sana peke yake bila jirani ya karibu sana. Mlima huwa na mfumo wa upepo ambako mchana upepo unaelekea juu na wakati wa usiku kuna upepo unaotelemka kutoka juu. Hii inatokea zaidi upande wa kusini kuliko upande wa kaskazini kwa sababu tako la mlima ni pana zaidi upande wa kusini na mitelemko yake inaelekea zaidi hivyo kuathiri tabianchi zaidi. [20].

Kilimanjaro huwa na majira mawili ya mvua, moja ya Machi hadi Mei na nyingine mnamo mwezi wa Novemba. Mitelemko ya kaskazini hupokea mvua chache kulingana na mitelemko ya kusini.[26]

Sehemu za chini za mtelemko wa kusini hupokea milimita za mvua 800 – 900 kwa mwaka. Kiwango hiki kinaongezeka kwa milimita 1,500 hadi 2,000 kwenye kimo cha mita 1,500 na hadi juu ya milimita 3,000 kwenye ukanda wa msitu kwa mita 2,000 hadi 2,300. Juu zaidi usimbishaji unapungua tena hadi milimita 200.[27]: 18 

Halijoto kwenye kilele ina wastani ya sentigredi -7 yaani jalidi. Halijoto juu ya ngao ya barafu upande wa kaskazini wakati wa usiku huwa na wastani wa sentigredi -9 na wakati wa mchana -4. Viwango vya chini vya -15 hadi -27 vimepimiwa pia.[28]: 674 

Usimbishaji wa theluji unaweza kutokea wakati wowote lakini kwa kawaida hutokea Zaidi wakati wa majira ya mvua. (Novemba–Desemba na Machi–Mei).[28]: 673  Usimbishaji wote kwenye kilele ni hasa theluji au mchnganyiko wa tehluji na mvua kwenye kiwango cha milimita 250 hadi 500 kwa mwaka na kuvukiza haraka.[29]

Barafu na barafuto

 
Theluji na barafu katika kilele cha mlima Kilimanjaro, 1993.

Mlima Kilimanjaro hujulikana kuwa kuwa ni mlima wa Afrika mwenye kofia ya barafu ya kudumu. Pamoja na Kilimanjaro kuna sehemu mbili nyingine tu barani Afrika, ni Ruwenzori na Mlima Kenya. Lakini kiasi cha barafu imepungua kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100. Mwingereza P.C. Spink aliona mwaka 1944 ya kwamba barafu ilipungua sana kulingana na taarifa aliyojua kutoka mpandaji wa kwanza Hans Meyer. Baina 1912 eneo la ngao ya barafu limepungua kutoka kilomita za mraba 12 hadi 1.85 km² kwenye mwaka 2009. Hii inalingana na kupunguzwa asilimia 85%. Sababu kuu ya mabadiliko haya ni kupungukiwa kwa kiwango cha usimbishaji katika mazingira ya mlima tangu mwisho wa karne ya 19.

Maana Kilimanjaro ni mlima wa juu vile ya kwamba mvua wote (pamoja na ukungu na usimbishaji mwingine) unaofika kwenye kilele chake utaganda na kuwa theluji. Theluji inayokaa muda mrefu tena katika ganda nene itakuwa barafu. Lakini wakati uleule mishale ya jua zinasababisha kupotea kwa theluji na barafu kwa njia ya uvukizaji. Kwa jumla kuongezeka au kupungukiwa kwa barafu kwenye kimo hiki ni swali la kiasi cha mvua na usimbishaji mwingine zinazofika hapa.

Leo hii kuna barafuto kwenye Kibo pekee pamoja na mabaki ya ngao ya barafu kwenye tambarare ya kilele na kwenye mitelemko ya Kibo. [30][31][32][33][34] http://www.jstor.org/stable/1788958?seq=1#page_scan_tab_contents Hii ngao ya barafu bado iko kwa sababu Kilimanjaro ni mlima usio na vilele vikali unaofika juu ya kimo cha mstari wa jeledi. Kasoko ya Kibo imepita na kukata ngao hiyo. [20]: 5  Siku hizi hakuna miendo ya maana inayoonekana kwenye barafuto za kilele kwa sababu unene wao imepungua mno..[29] Utafiti wa kijiolojia umeonyesha ya kwamba kulikuwa na vipindi vitano vya upanuzi wa barafuto katika miaka 500,000 iliyopita vilivyofuatwa na vipindi vya kupungua. [35]

Ngao ya barafu mfululizo ilifunika mlima wote hadi kimo cha mita 3,200 miaka 24,000 – 25,000 iliyopita wakati barafuto kote duniani zilienea sana. [14][36] Kuna dalili ya kwamba barafu yote mlimani iliwahi kupotea kabisa takriban miaka 11,500 iliyopita kutokana na ukame dunaini wakati ule.[29] Kuongezeka kwa usimbishaji wakati wa Holoseni (miaka 11,500 iliyopita) kumeruhusu kurudi kwa barafu mlimani. [29] barafuto ziliweza kudumisha kipindi cha ukame miaka 4,000 iliyopita. [29][37]

Wakati wa kutembelewa mara ya kwanza katika miaka ya 1880, kilele cha Kibo kilifunikwa kabisa kwa ngao ya barafu yenye eneo la kilomita za mraba 20 hivi na mikondo ya barafuto iliendelea wenye mitelemko ya kando. Isipokuwa pia ya kati, kaldera yote ilifunikwa na barafu.[14][36]

 
Kilele cha Kibo kilivyoonekana kutoka angani mwaka 1938.

Imetazamiwa ya kwamba barafuto kwenye mitelemko ilirudi nyuma haraka kuanzia 1912 hadi 1953, na polepole zaidi tangu wakati ule. Inaendelea kupungua nah ii inaonyesha ya kwamba bado hakuna uwiano kati ya kiasi cha mvua kinachofika kwenye kilele na uvukizaji nah ii inaonyesha mabadiliko ya tabianachi yanayoendelea. [14]

Pamoja na kufunika eneo dogo zaidi, yaani kujikaza, barafuto pia zimepungua unene kutokana na kuyeyuka na uvukizaji. [37][29] Mabadiliko haya kwenye barafuto za Kilimanjaro zinalingana na mabadiliko yanayoonekana kwenye barafuto kote duniani. [37] At the current rate, most of the ice on Kilimanjaro will disappear by 2040 and "it is highly unlikely that any ice body will remain after 2060".: 430 

Kama barafu juu ya Kilimanjaro ingepotea kabisa hii isingekuwa tatizo kubwa kwa maji yanayopatikana katika maeneo yanayozunguka mlima. Kiasi cha barafu juu ya mlima ni kidogo sana kuliko kiasi cha maji yanayohifadhiwa na misitu kwenye mitelemko ya mlima chini zaidi. Misitu hii ni chanzo cha maji yanayotiririke chini katika mito na vijito vya mlima mkubwa.[38]

Uoto

Kuna misitu asilia zinazofunika takriban kilomita ya mraba 1,000 kwenze mlima[26] .

Sehemu ya chini hulimwa kwa kupanda mahindi, maharagwe na alizeti, pia ngano upande wa magharibi. Kuna mabaki ya uoto wa savana ya awali yenye miti kama Acacia, Combretum, Terminalia na Grewia. Kuanzia kimo cha mita 1000 hadi mita 1800 kuna kilimo cha kahawa kwa namna ya kidesturi ya "Wachaga inayopanda miti na mazao kwa pamoja. Uoto asilia umebaki pekee katika mabonde majkali yasiyoweza kutumiwa kwa kilimo [39] na hapa ni tofauti na uoto kwenye maeneo ya juu zaidi.

Kuanzia kimo cha mita 1000 hadi mita 1800 kuna kilimo cha kahawa kwa namna ya kidesturi ya "Wachaga inayopanda miti na mazao kwa pamoja. Uoto asilia umebaki pekee katika mabonde majkali yasiyoweza kutumiwa kwa kilimo [39] na hapa ni tofauti na uoto kwenye maeneo ya juu Zaidi.

Kwenye mitelemko ya kusini penye mvua nyingi kuna misitu ya mvua yenye miti aina ya Ocotea usambarensis pamoja na kangaga na epipythi. Juu zaidi penye ukungu wa kudumu kuna Podocarpus latifolius, Hagenia abyssinica na Erica excelsa pamoja na kuvumwani.

Upande wa kaskazini ulio kavu zaidi pana misitu ya mizeituni, Croton-Mlungu-mbago (Calodendrum), Cassipourea (Mugome na Msikundazi) na Juniperus (Mtarakwa) kadri kimo kinaongezeka.

Juu zaidi kati ya mita 3,100 na 3,900 hufuata kanda la vichaka vya Erica (mdamba) na juu yake kunamajanimajani tu kama Helichrysum hadi mita 4500.[27][40]

Utafiti kwenye kasoko ya Maundi kwenye kimo cha mita 2780 umeonyesha ya kwamba uoto wa Kilimanjaro ulibadilika katika mwendo wa karne na milenia. Wakati wa baridi kwenye enzi ya barafu miaka 42,000 – 30,000 iliyopita misitu ilishuka chini na kanda la mdamba lilitokea takriban mita 1,500 chini ya hali yake ya sasa..[39]

Wanyama

Hakuna wanyama wakubwa wengi waliobaki mlimani. Wanapatikana hasa kwenye misitu na sehemu za chini mlimani. Tembo na nyati wanaweza kuwa na hatari kwa watalii wanaopanda mlima na pia kwa wakulima. Pongo, vinyonga, digidigi, paa, Nguchiro, nyani mbalimbali kama mbega, komba, chui, chozi na ngiri wametazamiwa pia. Punda milia na fisi wanapatikana mara chache kweye tambarare juu ya Shira.[41]

Kuna spishi chache zinazopatikana Kilimanjaro pekee hizi ni pamoja na “kirukanjia wa Kilimanjaro”[42] na spishi ya kinyonga kinachoitwa Kinyongia tavetana.[43]

Tazama pia

Marejeo

  1. 1.0 1.1 Johann Ludwig Krapf; Ernest George Ravenstein (1860). Travels, Researches, and Missionary Labours, During an Eighteen Years' Residence in Eastern Africa: Together with Journeys to Jagga, Usambara, Ukambani, Shoa, Abessinia and Khartum, and a Coasting Voyage from Nombaz to Cape Delgado. Trübner and Company, Paternoster Row. uk. 255.
  2. James Wood (1907). "Kilima-Njaro". 1907 Nuttall Encyclopædia of General Knowledge. fromoldbooks.org. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Through Masai land: a journey of exploration among the snowclad volcanic mountains and strange tribes of eastern equatorial Africa, authored by Johann Ludwig Krapf and Ernest George Ravenstein, Low, Marston, Searle, & Rivington, London, 1887
  4. "Perspective with Landsat Overlay". SRTM TANZANIA IMAGES. California Institute of Technology. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Johann Ludwig Krapf; Ernest George Ravenstein (1860). Travels, Researches, and Missionary Labours, During an Eighteen Years' Residence in Eastern Africa: Together with Journeys to Jagga, Usambara, Ukambani, Shoa, Abessinia and Khartum, and a Coasting Voyage from Nombaz to Cape Delgado. Trübner and Company, Paternoster Row. uk. 544.
  6. Briggs, Philip (1996): "Guide to Tanzania; 2nd edition." Bradt Guides.
  7. Haieleweki kama alitoa jina kwa heshima ya Kaisari Wilhelm I (aliyeunganisha Ujerumani) au mwanawe Kaisari Wilhelm II (aliyekuwa mtawala tangu mwaka 1888 tu)
  8. Demhardt, I.J.. "GERMAN CONTRIBUTIONS TO THE CARTOGRAPHY OF SOUTH WEST AND EAST AFRICA FROM MID 19th CENTURY TO WORLD WAR I". University of Technology Darmstadt. http://icaci.org/files/documents/ICC_proceedings/ICC2003/Papers/110.pdf. Retrieved 16 July 2015.
  9. P. C. Spink (1945). "Further Notes on the Kibo Inner Crater and Glaciers of Kilimanjaro and Mount Kenya". The Geographical Journal. 106 (5–6): 213. doi:10.2307/1788958. JSTOR 1788958.
  10. D. F. O. Dangar (1965). "Dangar Alpine Notes" (PDF). The Alpine Journal. 70 (310–311): 328.
  11. "Kilimanjaro National Park". World Heritage List. UNESCO World Heritage Centre. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Mt Kilimanjaro Volcano". Volcano Live - John Seach. Iliwekwa mnamo 22 Novemba 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. "Mawenzi". Peakware. Interactive Outdoors, Inc. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. 14.0 14.1 14.2 14.3 Nicolas J. Cullen, Thomas Mölg, Georg Kaser, Khalid Hussein, Konrad Steffen, and Douglas R. Hardy (2006). "Kilimanjaro Glaciers: Recent areal extent from satellite data and new interpretation of observed 20th century retreat rates" (PDF). Geophysical Research Letters. 33 (16). Bibcode:2006GeoRL..3316502C. doi:10.1029/2006GL027084.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  15. 15.0 15.1 15.2 15.3 15.4 15.5 15.6 15.7 Nonnotte, Philippe; Hervé Guillou; Bernard Le Gall; Mathieu Benoit; Joseph Cotten; Stéphane Scaillet (2008). "New K-Ar age determinations of Kilimanjaro volcano in the North Tanzanian diverging rift, East Africa" (PDF). Journal of Volcanology and Geothermal Research. 173 (1–2): 99–112. doi:10.1016/j.jvolgeores.2007.12.042. Iliwekwa mnamo 29 Julai 2015.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  16. "Mount Kilimanjaro National Park". Tanzania National Parks. Tanzania National Parks. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-09-23. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2015. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  17. 17.0 17.1 Pascal Sirguey, Nicolas J. Cullen and Jorge Filipe Dos Santos. "The New Digital Orthometric Elevation Model of Kilimanjaro" (PDF). CEUR Workshop Proceedings. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  18. 18.0 18.1 18.2 18.3 W. H. Wilcockson (1956). "Preliminary Notes on the Geology of Kilimanjaro". Geological Magazine. 93 (3): 218–228. doi:10.1017/S0016756800066590.
  19. 19.0 19.1 19.2 John Barry Dawson (2008). The Gregory Rift Valley and Neogene-recent Volcanoes of Northern Tanzania. Geological Society of London. uk. 56. ISBN 978-1-86239-267-0.
  20. 20.0 20.1 20.2 C. Gillman (1923). "An Ascent of Kilimanjaro". The Geographical Journal. 61 (1): 1–21. doi:10.2307/1780513. JSTOR 10.2307/1780513. {{cite journal}}: Unknown parameter |registration= ignored (|url-access= suggested) (help)
  21. "Gustav Otto Richard Reusch". Biographies. The Center for Volga German Studies at Concordia University. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-10-24. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  22. Richard Leider (10 Mei 2010). The Power of Purpose: Find Meaning, Live Longer, Better. Berrett-Koehler Publishers. uk. 12. ISBN 978-1-60509-527-1.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  23. "Kilimanjaro". Volcano World. Oregon State University. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  24. Alex Stewart (23 Aprili 2012). Kilimanjaro: A Complete Trekker's Guide: Preparations, practicalities and trekking routes to the 'Roof of Africa'. Cicerone Press Limited. uk. 100. ISBN 978-1-84965-622-1.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  25. William Dubois Newmark (1991). The Conservation of Mount Kilimanjaro. IUCN. ku. 105–106. ISBN 978-2-8317-0070-0.
  26. 26.0 26.1 Andreas Hemp (2006). "Continuum or zonation? Altitudinal gradients in the forest vegetation of Mt. Kilimanjaro" (PDF). Plant Ecology. 184 (1): 27–42. doi:10.1007/s11258-005-9049-4.
  27. 27.0 27.1 Andreas Hemp (2007). "Introduced plants on Kilimanjaro: tourism and its impact" (PDF). Plant Ecology. 197 (1): 17–29. doi:10.1007/s11258-007-9356-z.
  28. 28.0 28.1 Vijay P. Singh; Pratap Singh; Umesh K. Haritashya (1 Julai 2011). Encyclopedia of Snow, Ice and Glaciers. Springer Science & Business Media. ISBN 978-90-481-2641-5.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  29. 29.0 29.1 29.2 29.3 29.4 29.5 P. Gabrielli, D. R. Hardy, N. Kehrwald, M. Davis, G. Cozzi, C. Turetta, C. Barbante, L. G. Thompson (2014). "Deglaciated areas of Kilimanjaro as a source of volcanic trace elements deposited on the ice cap during the late Holocene" (PDF). Quaternary Science Reviews. 93 (1): 1–10. doi:10.1016/j.quascirev.2014.03.007.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  30. Brian Vastag: The melting snows of Kilimanjaro. In: Nature. 2009, doi:10.1038/news.2009.1055.
  31. Georg Kaser, Douglas R. Hardy u. a.: Modern glacier retreat on Kilimanjaro as evidence of climate change: observations and facts. In: International Journal of Climatology. 24, 2004, S. 329, doi:10.1002/joc.1008.
  32. Thomas Mölg: Solar-radiation-maintained glacier recession on Kilimanjaro drawn from combined ice-radiation geometry modeling. In: Journal of Geophysical Research. 108, 2003, doi:10.1029/2003JD003546.
  33. Thomas Mölg: Ablation and associated energy balance of a horizontal glacier surface on Kilimanjaro. In: Journal of Geophysical Research. 109, 2004, doi:10.1029/2003JD004338.
  34. N. J. Cullen, P. Sirguey, T. Mölg, G. Kaser, M. Winkler, S. J. Fitzsimons: A century of ice retreat on Kilimanjaro: the mapping reloaded. The Cryosphere Discuss., 2012, 6, 4233-4265, doi:10.5194/tcd-6-4233-2012.
  35. Bryan G. Mark and Henry A. Osmaston (2008). "Quaternary glaciation in Africa: Key chronologies and climatic implications" (PDF). Journal of Quaternary Science. 23: 589–608. doi:10.1002/jqs.1222.
  36. 36.0 36.1 Young, James A. T. "Glaciers of the Middle East and Africa" (PDF). U.S. Geological Professional Survey. U.S. Department of the Interior. ku. G61, G58, G59 G62. Iliwekwa mnamo 16 Agosti 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  37. 37.0 37.1 37.2 L. G. Thompson, H. H. Brecher, E. Mosley-Thompson, D. R. Hardy, B. G. Mark (2009). "Glacier loss on Kilimanjaro continues unabated". Proceedings of the National Academy of Sciences. 106 (47): 19770–5. doi:10.1073/pnas.0906029106. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-02-08. Iliwekwa mnamo 2016-04-01. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  38. Georg Kaser, Thomas Mölg, Nicolas J. Cullen, Douglas R. Hardy, Michael Winkler, Rainer Prinz, and Lindsey Nicholson. "East African glacier loss and climate change: Corrections to the UNEP article Africa without ice and snow" (PDF). 6: 1–6. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  39. 39.0 39.1 39.2 Lisa Schüler, Andreas Hemp, Wolfgang Zech, Hermann Behling (2012). "Vegetation, climate and fire-dynamics in East Africa inferred from the Maundi crater pollen record from Mt Kilimanjaro during the last glacial–interglacial cycle". Quaternary Science Reviews. 39: 1–13. doi:10.1016/j.quascirev.2012.02.003 – kutoka ScienceDirect.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  40. L. A. Bruijnzeel; F. N. Scatena; L. S. Hamilton (6 Januari 2011). Tropical Montane Cloud Forests: Science for Conservation and Management. Cambridge University Press. uk. 136. ISBN 978-1-139-49455-7.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  41. Cameron M. Burns (2006). Kilimanjaro & East Africa: A Climbing and Trekking Guide. The Mountaineers Books. uk. 50. ISBN 978-0-89886-604-9.
  42. "Crocidura monax". IUCN Red List of Threatened Species. International Union for Conservation of Nature and Natural Resources. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-24. Iliwekwa mnamo Agosti 15, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  43. "Kinyongia tavetana (STEINDACHNER, 1891)". The Reptile Database. Zoological Museum Hamburg. Iliwekwa mnamo 15 Agosti 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

 
WikiMedia Commons