NARC-Kenya

National Rainbow Coalition–Kenya (NARC-Kenya) ni chama cha kisiasa nchini Kenya. Kilianzishwa kama farakano katika NARC asilia baada ya kura maalumu juu ya katiba ya Kenya 2005.

NARC-Kenya ilipangwa kuwa chama kipya cha kumrudisha Mwai Kibaki kama rais wa Kenya baada ya kuporomoka kwa NARC asilia bila kuacha nembo na jina la "Rainbow".

NARC-Kenya ilikuwa na mafanikio mwaka 2006 katika uchaguzi mdogo ilipopata viti vitatu. Lakini baadaye ilionekana ya kwamba sehemu ya wanaisasa katika serikali ya Kibaki walikataa kuijiunga na chama wakidai athira ya viongozi wa Kenya ya Kati ilikuwa kubwa mno ilikuwa kama umbo tofauti ya Democratic Party of Kenya.

Hivyo Oktoba 2007 miezi michache kabla ya uchaguzi maungano mapya ya Party of National Unity yaliundwa kuwa chombo cha kempeni ya Kibaki.

Narc Kenya iliamua awali kujiunga katika PNU. Kwenye uchaguzi ilipeleka wagombea kadhaa chini ya bendera yake ikashinda viti vitatu na kungina bungeni.

Viungo vya NjeEdit