Alpha Gruis, α Gruis, Alnair Nairi

Nairi (Alfa Gruis, Alnair)
Kundinyota Kuruki (Grus)
Mwangaza unaonekana 1.7
Kundi la spektra B6 V
Paralaksi (mas) 32.29 ± 0.21
Umbali (miakanuru) 101
Mwangaza halisi -0.72
Masi M☉ 4
Nusukipenyo R☉ 3.4
Mng’aro L☉ 263
Jotoridi usoni wa nyota (K) 13920
Majina mbadala Al Na'ir, α Gru, CD−47° 14063, FK5 829, GCTP 5339.00, Gl 848.2, HD 209952, HIP 109268, HR 8425, SAO 230992

Nairi (ar., lat. & ing. Alnair pia α Alfa Gruis [1], kifupi Alfa Gru, α Gru) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Kuruki (Grus) na nyota angavu ya 31 kwenye anga ya usiku.

Nairi inayomaanisha “ng'avu” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema النّيّر al-nair wakimaanisha „ ng'avu ". Waarabu walihesabu nyota hii katika kundi la Hutu Junubi. Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Alnair" [3] .

Alfa Gruis ni jina la Bayer kwa sababu Alfa ni herufi ya kwanza katika Alfabeti ya Kigiriki na Nairi ni nyota angavu zaidi katika Kuruki - Grus.

Nairi iko umbali wa miakanuru takriban 101 kutoka Jua letu. Ina mwangaza unaoonekana wa mag 1.7 na mwangaza halisi ni -0.72. Spektra yake ni ya aina ya B6[4] au B7 [5]. "B" inamaanisha ni nyota ya safu kuu inayoyeyunganisha hidrojeni kuwa heliamu; inawezekana imeshafika tayari mwisho wa hatua hii na itahamia karibuni kuyeyunganisha heli kwa elementi nzito zaidi.

Kama nyota nyingi zinazofanana nayo inazunguka haraka kwenye mhimili wake kwa kasi ya angalau kilomita 236 kwa saa katika kanda ya ikweta yake.[6]

Tanbihi

hariri
  1. Gruis ni uhusika milikishi (en:genitive) wa "Grus" katika lugha ya Kilatini na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa, Beta, Gamma Gruis, nk.
  2. ling. Knappert 1993
  3. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
  4. Gray, R. O.; et al. (July 2006), uk. 51 (HIP 109268)
  5. Malagnini, M. L.; Morossi, C. (November 1990), uk. 1018 (HD 209952)
  6. Kaler, Al Nair

Viungo vya Nje

hariri


Marejeo

hariri
  • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 331 (online kwenye archive.org)
  • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Lane, Edward William : An Arabic - English Lexicon by in eight parts – 1872 (Grus Collection Arabic Materials Digitized Text Version v1.1 of reprint Beirut – Lebanon 1968) online hapa
  • Gray, R. O.; et al. (July 2006), "Contributions to the Nearby Stars (NStars) Project: spectroscopy of stars earlier than M0 within 40 pc-The Southern Sample", The Astronomical Journal, 132 (1): 161–170 online hapa
  • Hoffleit, D.; Warren, W. H. Jr. "HR 8425, database entry". The Bright Star Catalogue (5th Revised (Preliminary) ed.). CDS. Retrieved 5 September 2015. online hapa
  • Malagnini, M. L.; Morossi, C. (November 1990), "Accurate absolute luminosities, effective temperatures, radii, masses and surface gravities for a selected sample of field stars", Astronomy and Astrophysics Supplement Series, 85 (3): 1015–1019, online hapa