Nako 2 Nako
Nako 2 Nako (Nako to Nako, N2N au Nako 2 Nako Soldiers) ni kundi la hip hop kutoka Kaskazini mwa Tanzania - Arusha. Kundi linaundwa na wanachama wanne (4) ambao ni Lord Eyez, G Nako, Ibra da Hustler na Bou Nako. Msanii Ibra da Hustler alijitoa kwenye kundi mwezi wa 11, mwaka 2008 kutokana na kupishana maelewano na wanamuziki wenzake kwenye kundi. Hivyo, Ibra da Hustler anaendelea kufanya muziki wake mwenyewe pasipo kua na kundi (solo artist). Jina la 'nako 2 nako lilipatikana katika gym ya mazoezi (maarufu kama dojo) ambayo iliwakutanisha wanamziki hawa wakiwa wanafanya mazoezi. Kundi hili pia linaundwa na wasanii wengine ambao bado hawajapata umaarufu sana (Junior nakos) pamoja na wanakikundi wengine wasio wanamziki, yaani jumuia ya wanamazoezi wa gym ambayo mazoezi ya dojo yalikua yakifanyika.
Kwa muda mrefu kundi hili limeonyesha uwezo mkubwa katika kuwakilisha muziki wa kizazi kipya aina ya rap au hip hop. Nako 2 Nako wamepata umaarufu kwa ustadi wao wa kughani kwa kutumia Lugha ya Kiswahili.
Baadhi ya nyimbo zao maarufu
hariri- Ndio Zetu Kuwakilisha 2005
- Bang 2007
- Hawatuwezi 2005
- Bang Rmx 2008
- Mchizi Wangu 2008
- Hakuna Mahali Kama 2008
- Hiphop 2008
- Iko Wazi 2009
- Mpango Mzima 2010
- Wawiwo 2010
- Katikati 2010
- Hardcore 2018
Na bado tunazidi
Viungo vya Nje
haririMakala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nako 2 Nako kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |