Namanga ni mji ambao uko kusini mwa Kenya, kwenye kaunti ya Kajiado mpakani mwa Tanzania[1].

Majengo ya shule katika Mji wa Namanga, Kenya.

Mji huu upo kilomita 200 kutoka Nairobi na kilomita 130 kutoka mji wa Arusha (Tanzania).

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 ulikuwa na wakazi 14,922[2].

Uchumi wa mji huu unategemea sana utalii. Watalii wengi wanaotembelea wanyama wa Hifadhi ya Taifa ya Amboseli hupitia kwenye mji huu.

Mlima Kilimanjaro unaonekana kusini mwa mji huu. Pia mlima Oldoinyo Orok uko kaskazini magharibi kwa mji huu na hujulikana kama milima ya Namanga.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri

2°33′S 36°47′E / 2.550°S 36.783°E / -2.550; 36.783