Ndege wa Peponi
Ndege wa Peponi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Ndege wa Peponi (Paradisaea apoda)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Ndege wa Peponi (en:Bird-of-paradise) ni ndege wa familia ya Paradisaeidae ambao ni wadogo wakiwa maarufu kwa manyoya yao marefu na yenye rangi nyingi. Wanaishi huko Indonesia, Papua New Guinea na Australia ya Mashariki. Wanaojulikana zaidi ni hao wa jenasi Paradisaea pamoja na spishi ya Paradisaea apoda.
Paradisaea apoda alipokea jina "apoda" (bila miguu) kwa sababu Linnaeus aliamini ndege hao hawana miguu. Sababu yake inaaminiwa kuwa mifano ya kwanza ilitumwa kwa miguu iliyokatwa. Kwa hiyo ndege hao wenye rangi za kuvutia waliaminiwa kuwa "ndege kutoka peponi" au kutoka paradiso wasiohitaji kugusa ardhi wala matawi ya miti.
Kundinyota la Ndege wa Peponi lilipokea jina lake la Kigiriki "Apus" (bila miguu) kutokana kwa ndege hizi.