New Black Panther Party for Self Defence

New Black Panther Party for Self-Defense ni kundi la wanaharakati weusi wenye siasa kali na mwamko wa kimapinduzi nchini Marekani. Kundi hili lilianzishwa mwaka 1989 na mtangazaji wa redio, Aaron Michaels, huko Dallas, Texas. Mwanzoni kundi hili lilichukua jina la "Black Panther Party" ambalo lilikuwa ni jina la kundi jingine lililokuwa na itikadi za kimapinduzi nchini Marekani. Wanachama wa kundi la mwanzo la Black Panther walipinga matumizi ya jina hilo yanayofanya na kundi jipya la Aaron Michaels. Michaels na wenzake walidai kuwa Black Panther haikuwa mali ya mtu binafsi bali jamii nzima ya watu weusi, hivyo hakuna ubaya jina hilo likatumika. Hata hivyo waliamua kuongeza neno "New" katika jina hilo.

Faili:Nbplogo.png
Kikundi cha watu weusi huko Marekani

Kundi hili linakua huku likifungua matawi sehemu mbalimbali nchini Marekani. Wafuasi wengi waliojitenga na kundi jingine la Nation of Islam walijiunga na kundi hili wakimfuata aliyekuwa kiongozi wa New Black Panther Party, marehemu Khalid Abdul Muhammad. Khalid Abdul Muhammad alikuwa ni mhubiri wa Nation of Islam kabla hajajiunga na New Black Panther Party.

Falsafa za kundi hili ni mchanganyiko wa mahubiri ya Malcolm X, Marcus Garvey, itikadi za uzalendo wa Kiafrika, na uanaharakati wa kimapinduzi.