Ngalula ni jina la kutaja wimbo uliotungwa na kuimbwa na kundi zima la Marquis Original katika miaka ya tisini. Moja kati ya nyimbo zilizotamba sana katika miaka hiyo. Mashairi yake anazungumzia uvumilivu katika ndoa. Hasa pamoja na vituko vyake lakini atakuwa naye pia maishani. Yupo njia panda katika maamuzi haya ambayo anayajua yeye mwenyewe licha ya vituko vyote anavyofanyiwa. Kisa tu amemzoea na anamuelewa vizuri kuliko mtu yeyote, shida na raha zake anazielewa na anazivumilia. Baadaye, anamsihi azibe masikio kwa vile hayo ni maji ya moto yatapoa tu, mama. Humu walitumia sana mtindo wa "Sendema" mtindo maarufu sana kwa bendi hii. Kama ilivyo kawaida wa muziki wa dansi, sehemu kubwa inapiga vyombo tupu kama tumbuizo kwa wasikilizaji. Midomo ya bata (tarumbeta) zimepigwa vilivyo katika wimbo huu - kwa umahiri wa hali ya juu.

"Ngalula"
Wimbo wa Marquis Original
Umetolewa 1990-1991
Umerekodiwa 1989-1990
Aina ya wimbo Muziki wa dansi
Lugha Kiswahili
Urefu 6:27

Viungo vya Nje

hariri