Ngao ya Jamii ni mashindano unaoashiria ufunguzi wa msimu mpya wa michezo yanayofanyika mara moja kwa mwaka unazozikutanisha mshindi wa msimu wa nyuma wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mshindi wa Kombe la FA Tanzania. Ikiwa mshindi wa Ligi kuu ndiye mshindi wa Kombe la FA, mpinzani atakuwa aliyeshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi. Mashindano hayo yanatambulika rasmi na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF).[1][2][3][4]

Mabadiliko ya Mfumo

hariri

Kuanzia msimu wa 2022/23, TFF ilitangaza mabadiliko kwenye mfumo wa mchezo wa ngao ya Jamii. TFF ilbadilisha kanuni ya (19:1) kuhusu mchezo wa Ngao ya jamii ambapo kwa sasa kutakuwa na shindano la Ngao ya Jamii na sio mchezo mmoja[5]. Mfumo huu mpya unamaanisha kutakua na michezo ya nusu fainali na fainali. Michezo ya Nusu fainali ingezikutanisha Mshindi wa Ligi dhidi ya aliyeshika nafasi ya tatu kwenye msimamo, na Aliyeshika nafasi ya pili dhidi ya aliyeshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi. Timu za Young Africans, Simba, Azam na Singida big Starts ndizo zilizokua za kwanza kushiriki kwenye mfumo huu mpya, na Simba ndio timu ya kwanza kushinda taji la Ngao ya Jamii kwa kutumia mfumo huu.[6][7]

Washindi

hariri
Mwaka Mshindi Matokeo Mshindani Tanbihi.
2001 Young African 2–1 Simba
2002 Simba 4–1 Young African
2003 Simba 1–0 Mtibwa Sugar
2004 Haikuchezwa
2005 Simba 2–0 Young African
2006 Haikuchezwa
2007
2008
2009 Mtibwa Sugar 1–0 Young African
2010 Young African 0–0

[3–1 pen]

Simba
2011 Simba 0–0 Young African
2012 Simba 3–2 Azam
2013 Young African 1–0 Azam
2014 Young African 3–0 Azam
2015 Young African 0–0

[8–7 pen]

Azam
2016 Azam 2–2

[4–1 pen]

Young African
2017 Simba 0–0

[5–4 pen]

Young African
2018 Simba 2–1 Mtibwa Sugar
2019 Simba 4–2 Azam
2020 Simba 2–0 Namungo [8]
2021 Young African 1–0 Simba
2022 Young Africans 2–1 Simba
2023 Simba 0–0

[3–1 pen]

Young Africans
2024 Young Africans 4–1 Azam

Source: RSSSF[9]

Tanbihi

hariri
  1. "Simba edge Namungo to clinch Tanzania Community Shield". CAFOnline.com (kwa Kiingereza). CAF-Confedération Africaine du Football. Iliwekwa mnamo 2021-09-29.
  2. "Yanga beat Simba to lift the Community Shield". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-09-25. Iliwekwa mnamo 2021-09-29.
  3. "TFF Community Shield – TFF" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-09-29.
  4. "Tanzania Community Shield: Francis Kahata scores as Simba SC floor Azam FC". www.goal.com. Goal. Iliwekwa mnamo 2021-09-29.
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-11-13. Iliwekwa mnamo 2024-11-12.
  6. https://spotileo.co.tz/ngao-ya-jamii-msimu-huu-itakuwa-na-msisimuko/
  7. https://trtafrika.com/sw/sports/simba-sc-bingwa-kombe-la-ngao-ya-jamii-2023-14470104
  8. "Simba SC clinched Community Shield title over Namungo FC". Africa Top Sports. 31 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 2 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Tanzania - List of Cup Winners". RSSSF. Iliwekwa mnamo 2021-09-30.