Ngurunguru
Dume la ngurunguru (Oreotragus oreotragus)
Dume la ngurunguru
(Oreotragus oreotragus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyana wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J. E. Gray, 1821
Nusufamilia: Antilopinae (Wanyama wanaofanana na swala)
Jenasi: Oreotragus (Ngurunguru)
A. Smith, 1834
Spishi: O. oreotragus
(Zimmermann, 1783)
Ngazi za chini

Nususpishi 11:

Msambao wa ngurunguru
Msambao wa ngurunguru

Ngurunguru au mbuzi mawe (Oreotragus oreotragus) ni swala wadogo wanaotokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Jina “mbuzi mawe” ni kielekezi cha makazi yao: maeneo yenye mawe na majabali mengi. Swala hawa ni wadogo wenye kimo cha sm 58 begani. Wana rangi ya kahawa hadi kijivu, karibu na zaituni, na vidoa vidogo vingi. Rangi hii inafanana na rangi ya majabali ambapo wanaishi na kwa sababu ya hii hawaonekani vizuri kutoka umbali mkubwa. Madume wana pembe za sm 10–15. Katika Afrika ya Mashariki majike wana pembe pia mara nyingi. Wanyama hawa wasimama kwa ncha za kwato zao na wanaweza kubana kwato nne zote juu ya kipande cha jabali kwa upana wa sarafu kubwa. Hula mimea inayomea kati ya majabali. Hawana haja ya kunywa, kwa sababu hupata maji ya kutosha kutoka chakula chao.

Nususpishi hariri

  • Oreotragus oreotragus, Ngurunguru (Klipspringer)
    • Oreotragus o. aceratos, Ngurunguru wa Tanzania Kusi (msambao: Tanzania, Msumbiji, Malawi, Zambia, Angola)
    • Oreotragus o. aureus, Ngurunguru wa Kenya (msambao: Kenya)
    • Oreotragus o. centralis, Ngurunguru wa Zambia (msambo: Afrika ya Kati na ya Kusini)
    • Oreotragus o. oreotragus, Ngurunguru wa Rasi (msambao: Afrika Kusini)
    • Oreotragus o. porteousi, Ngurunguru wa Kati (msambao: Nijeria, Jamhuri ya Afrika ya Kati)
    • Oreotragus o. saltatrixoides, Ngurunguru wa Ethiopia (msambao: Uhabeshi, Eritrea, Jibuti, Sudani)
    • Oreotragus o. schillingsi, Ngurunguru Masai (msambao: Afrika ya Mashariki)
    • Oreotragus o. somalicus, Ngurunguru Somali (msambao: kaskazini mwa Somalia)
    • Oreotragus o. stevensoni, Ngurunguru wa Stevenson (msambao: Zimbabwe)
    • Oreotragus o. transvaalensis, Ngurunguru wa Transvaal (msambao: maneneo ya juu na Drakensberge ya Afrika Kusini)
    • Oreotragus o. tyleri, Ngurunguru wa Namibia (msambao: Namibia)
 
Jike la ngurunguru

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ngurunguru kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.