Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Tuzo ya Mwalimu Nyerere
Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kwa Kiingereza Order of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere) ni tuzo ya heshima zaidi nchini Tanzania.[1]. Tuzo hiyo ilipewa jina hilo ili kumuenzi rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.
Historia
haririTuzo hiyo ilianzishwa na Jakaya Mrisho Kikwete mnamo Desemba 2011, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara, ambayo kabla ya hapo ilikuwa ikijulikana kama Tanganyika.
Tanbihi
haririMakala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |