Heshima
Heshima (kutoka neno la Kiarabu) ni kitu anachopewa mtu kama alama ya kuthaminiwa kwake. Kwa maana nyingine ni thamani ya utu (utukufu, daraja la juu au jaha).
Heshima inadaiwa na wenye cheo na mamlaka, kuanzia wazazi kutoka kwa watoto wao.
Pia heshima inatarajiwa na watu wenye sifa na maadili bora.
Heshima kuu ni ile anayoistahili Mwenyezi Mungu tu na ambayo inaitwa ibada.
Heshima mara nyingi inaendana na usikivu na utiifu.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Heshima kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |