Nyakabindi ni kata ya Wilaya ya Bariadi Mjini katika Mkoa wa Simiyu, Tanzania, yenye postikodi namba 39121 [1].

Kata ya Nyakabindi inaundwa na vijiji vitano ambavyo ni Nyakabindi, Gagabali, Old Maswa, Bupandagila na Mwakibuga.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 27,573 [2]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 19,723 waishio humo.

Kata ina shule tano za msingi ambazo ni Nyakabindi s/m, Oldmaswa s/m, Bupandagila s/m, Mwakibuga A na Mwakibuga B s/m. Pia kuna shule mbili za sekondari za serikali ambazo ni Nyakabindi Sekondari na Old Maswa Sekondari, tena kuna shule moja ya sekondari ya binafsi iitwayo Bupandagila High School na inayomilikiwa na Kanisa la Wasabato Tanzania.

Marejeo hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01. 
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 219
  Kata za Wilaya ya Bariadi MjiniMkoa wa Shinyanga - Tanzania  

Bariadi | Bunamhala | Guduwi | Isanga | Malambo | Mhango | Nyakabindi | Nyangokolwa | Sima | Somanda


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Simiyu bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.