Wasabato
Wasabato ni Wakristo wanaomuabudu Mungu hasa siku ya Sabato, kama ilivyo kwa Wayahudi, tofauti na Wakristo walio wengi (99%) wanaoadhimisha tangu kale Jumapili kama siku ya ufufuko wa Yesu ambayo umeanza uumbaji mpya utakaofanya viumbehai kushiriki utukufu wa Mwana wa Mungu.
Kati ya madhehebu ya namna hiyo, maarufu zaidi ni Waadventista Wasabato ambao wamefikia kuwa milioni 17 duniani kote. Waadventista wa Sabato wanaamini katika Sabato kuwa ndilo pumziko pekee alilopumzika Mwenyezi Mungu (Mwanzo 2:2-3). Mara baada ya kuitakasa siku aliyopumzika alitoa agizo la kukumbukuka, kuheshimu na kuenzi siku hiyo ili iwe ukumbusho na agano la wanadamu na Mungu kama wanavyoamini Wasabato. Imani yao ilianzishwa miaka ya 1850 na mwanamke aitwaye Ellen G. White nchini Marekani akidai yeye ni nabii wa Mungu. Wasabato hao wanamwita nabii Ellen G. White
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wasabato kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |