Nyamwaga
Nyamwaga ni kata ya Wilaya ya Tarime katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31417 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,917 waishio humo. [2]
Katika eneo la kata kuna migodi ya dhahabu ya North Mara Gold Mine inayomilikiwa na kampuni Acacia Mining kutoka Uingereza. Nyamwaga ina vijiji vitano vinavyoiunda: 1. kijiji cha Nyamwaga 2. kijiji cha Komarera 3. kijiji cha Keisangora 4.kijiji cha Kimusi 5.kijiji cha Gwitare.
Diwani wa kata ya nyamwaga 2015/2020 ni Moses Matiko Misiwa kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime inayoundwa na kata 26.
Marejeo hariri
Kata za Wilaya ya Tarime Vijijini - Mkoa wa Mara - Tanzania |
||||
---|---|---|---|---|
Binagi * Bumera * Ganyange * Gorong'a * Gwitiryo * Itiryo * Kemambo * Kibasuka * Kiore * Komaswa * Kwihancha * Manga * Matongo * Mbogi * Muriba * Mwema * Nyakonga * Nyamwaga * Nyansincha * Nyanungu * Nyarero * Nyarokoba * Pemba * Regicheri * Sirari * Susuni
|