Nyimbo za Kiinjili
Nyimbo za Kiinjili (kwa Kiingereza Gospel music au Gospel songs) ni aina ya muziki wa Kikristo ambayo inatofautiana kadiri ya utamaduni na jamii zinapopatikana.
Lengo la nyimbo hizo linaweza kuwa uzuri zaidi, uenezi wa dini au hata ibada, lakini pia burudani na biashara.
Kwa kawaida zinategemea hasa sauti za waimbaji kuliko ala za muziki.
Asili ya mtindo huo ni mwanzo wa karne ya 17[1] katika jamii zenye asili ya Afrika.[2]
Kati ya watunzi wa awali kuna George Frederick Root, Philip Bliss, Charles H. Gabriel, William Howard Doane na Fanny Crosby.
Uenezi wa redio katika miaka ya 1920 ilichangia sana nyimbo hizo kujulikana na kupendwa sehemu nyingi za dunia.
Tanbihi
hariri- ↑ "Gospel History Timeline". University of Southern California. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-09-05. Iliwekwa mnamo Januari 31, 2012.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Jackson, Joyce Marie. "The changing nature of gospel music: A southern case study." African American Review 29.2 (1995): 185. Academic Search Premier. EBSCO. Web. October 5, 2010.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyimbo za Kiinjili kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |