Utamaduni ni jinsi binadamu anavyokabili maisha katika mazingira yake.[1] Hiyo inajumlisha ujuzi, imani, sanaa, maadili, sheria, desturi n.k. ambavyo mtu anajipatia kama mwanajamii.[2]

Michoro ya miambani huko Gobustan, Azerbaijan, 10000 KK ikionyesha utamaduni uliostawi.
Sanaa ya Misri ya kale, 1400 KK.
Dini na sanaa ni sehemu muhimu ya utamaduni wa binadamu.

Kama sifa maalumu ya binadamu, inayomtofautisha na wanyama, utamaduni ni suala la msingi katika anthropolojia, ukihusisha yale yote yanayopokezwa katika jamii fulani, kama vile lugha inayounganisha watu wanaohusika nao, fasihi, mafungamano, ndoa, michezo, ibada, sayansi na teknolojia.[3]

Utamaduni ulioendelea unaitwa pia "ustaarabu".

Kila utamaduni unabadilikabadilika mfululizo: ndani ya watu husika, baadhi wanachangia na kuunga mkono mabadiliko, wakati wengine wanayakataa. Ujuzi mpya na teknolojia, pamoja na mahitaji ya uchumi, ni kati ya mambo yanayosukuma zaidi kubadili kiasi fulani utamaduni.

Ufafanuzi

hariri

Neno la Kilatini lenye maana ya utamaduni ni Cultura ambalo lina usuli wake katika neno colere, linalomaanisha "kulima, kustawisha".[4] Neno hili linafafanuliwa namna nyingi. Kwa mfano, mwaka 1952, Alfred Kroeber na Clyde Kluckhohn walikusanya orodha ya vijelezi 164 vya neno hilo katika kazi yao: Culture:a Critical Review of Concepts and Definitions.[5]

Hata hivyo linatumika kimsingi katika njia tatu zifuatazo:

  • Maonjo ya hali ya juu katika sanaa, vilevile hujulikana kama utamaduni wa juu
  • Mkusanyo wa maarifa, itikadi na tabia ya binadamu ambao hutegemea sana uwezo wa kuwasilisha mawazo na mafunzo ya kijamii kwa njia ya ishara
  • Jumla ya mitazamo, kaida, malengo na maadili yanayotambulisha asasi, shirika au kikundi fulani

Historia ya dhana

hariri

Dhana hii ilipoibuka kwanza katika karne ya 18 na 19 barani Ulaya, ilimaanisha mchakato wa kulima au kuboresha kilimo au kilimo cha mboga. Katika karne ya 19 dhana hii ilimaanisha kuboreshwa kwa mja kupitia elimu na hali kadhalika ilimaanisha kutekelezwa kwa maazimio au maadili ya kitaifa.

Katikati ya karne ya 19, wanasayansi wengine walitumia dhana ya utamaduni kurejelea uwezo wa kiubia wa binadamu.

Katika karne ya 20, "utamaduni" ulijitokeza kama dhana ya msingi katika somo la Anthropolojia. "Utamaduni" ulihusisha mambo yote ya binadamu ambayo hayakufungamana na maumbile.

Dhana ya utamaduni katika Anthropolojia ya Kimarekani ilikuwa na maana mbili:

  • (1) Uwezo wa binadamu wa kuainisha na kuwasilisha tajiriba za kibinadamu kiishara na kutenda mambo kwa ubunifu; na
  • (2) Namna mbalimbali ambazo watu wanaoishi katika sehemu mbalimbali ulimwenguni huainisha na kuwasilisha tajiriba zao za maisha na kutenda mambo kwa ubunifu. Kufuatia vita vya pili vya dunia, dhana hii ilipata umaarufu, ingawa kwa fafanuzi tofautitofauti katika taaluma kama vile sosholojia, mafunzo ya utamaduni, saikolojia ya mipangilio na mafunzo ya usimamizi.

Dhana za karne ya 19

hariri
 
Johann G. Herder alitia maanani utamaduni wa kitaifa.
 
Adolf Bastian alikuza mtazamo wa kimataifa.

Ulimbwende wa Kijerumani

hariri

Mwanafalsafa wa Ujerumani Immanuel Kant (1724-1804) aliibuka na ufafanuzi wa binafsi wa "Falsafa ya mwangaza" akiulinganisha na dhana ya bildung: "kulingana naye, enzi ya nuru ni kule kutoka kwa binadamu katika hali ya uchanga."[6] Alielezea ya kwamba hali ya uchanga haitokani na kukosa kuelewa bali hutoka katika kukosa ujasiri wa kufikiria huria. Kutokana na hali hii ya woga wa kiusomi, Kant alihimiza: Sapere aude, "thubuthu kuwa na hekima!"

Johann Gottfried Herder (1744-1803) alielezea ubunifu wa binadamu kuwa muhimu kama kufikiria kwake ingawa hudhihirika katika njia mbalimbali. Herder alipendekeza namna ya pamoja ya bildung: "kulingana na Herder, bildung ni “jumla ya tajiriba ambazo hutoa utambulisho thabiti na dhana ya pamoja ya majaaliwa ya watu.”[7]

Mnamo mwaka 1795, mwanaisimu na mwanafalsafa Wilhelm Von Humboldt (1767-1835) alitoa wito kuanzisha anthropolojia ambayo iunganishe mawazo ya Kant na Herder. Katika enzi ya Kilimbwende, wasomi wa Kijerumani, hasa wale walioshughulikia muungano wa kitaifa - kama vile mapambano ya kitaifa ya kuanzisha dola la Ujerumani kutoka kwa vidola vidogovidogo na mapambano ya kitaifa ya makabila madogo dhidi ya himaya ya Austria-Hungaria - walikuza dhana ya utamaduni ya "mwonoulimwengu". Kulingana na shule hii ya mawazo, kila kabila lina mwonoulimwengu wake ambao hauwezi kulinganishwa na mionoulimwengu ya makundi mengine ya watu. Ingawa maoni hayo yalikuwa husishi kuliko maoni ya hapo awali, mwelekeo huu kuhusu utamaduni bado ulikuwa na milinganisho ya "ustaarabu" na "ushenzi" au tamaduni za "kikabila".

Mnamo mwaka 1860, Adolf Bastian (1826-1905) alipigania "umoja wa binadamu kisaikolojia". Alipendekeza kwamba, mlinganisho wa kisayansi wa jamii zote za binadamu udhihirishe mionoulimwengu tofauti inayojumuisha elementi sawa za kimsingi. Kulingana na Bastian, jamii zote za binadamu zina "mawazo sawa ya kimsingi" (Elementargedanken); tamaduni sawa au tofauti za "mawazo ya jadi" (Volkergedanken), haya ni mabadiliko ya kienyeji yanayofanyiwa mawazo ya kimsingi.[8] Ufafanuzi huu umechangia pakubwa kuelewa utamaduni siku hizi. Franz Boaz (1858-1942) alipata mafunzo katika utamaduni huu na ndiye aliyeyapeleka mawazo haya Marekani alipohamia kutoka Ujerumani.

Ulimbwende wa Kiingereza

hariri
 
Mshairi na mwandishi wa insha wa Uingereza Matthew Arnold alitumia neno "utamaduni" kumaanisha hali ya juu sana ya ubora wa binadamu.

Katika karne ya 19, mshairi na mwandishi wa insha wa Uingereza Matthew Arnold (1822-1888) alitumia neno utamaduni kumaanisha hali ya juu sana ya ubora wa binadamu, bora zaidi iliyowahi kuwaziwa na kusemwa ulimwenguni."[9] Dhana hii ya utamaduni inaweza kulinganishwa na dhana ya Kijerumani ya bildung: “utamaduni ukiwa ndio hali ya kutafuta ubora kupitia njia ya kufahamu kuhusu masuala yote yanayotuhusu, yale bora ambayo yamewazwa na kusemwa ulimwenguni.”[9]Kimsingi, utamaduni ulirejelea maadili ya juu ya kiusomi na ambayo yalihusishwa na sanaa, muziki wa kale na upishi wa hali ya juu. [10] Kama fomu hizo zilikuwa Urbane yanayohusiana na maisha, "utamaduni" ilikuwa kutambuliwa kwa "ustaarabu" (kutoka lat. civitas, mji). Facet mwingine wa harakati alikuwa Romantic riba katika Folklore, ambayo imesababisha kubaini "utamaduni" miongoni mwa wasio wasomi. Tofauti hii ni mara nyingi wanaotambuliwa kama kwamba kati ya "high utamaduni", yaani ile ya kundi tawala kijamii, na "Asili utamaduni". Kwa maneno mengine, dhana ya "utamaduni" kwamba maendeleo katika Ulaya wakati wa 18 na 19 mapema ya karne Ulaya speglas usawa ndani ya jamii.[11]

Matthew Arnold alilinganisha "utamaduni" na "fujo"; Wazungu wengine wakiwaiga wanafalsafa Thomas Hobbes na Jean-Jacques Rousseau walilinganisha "utamaduni" na "hali ya maumbile au hali ya nyikani". Kulingana na Hobbes na Rousseau, Waamerika asilia, ambao walitawaliwa na Wazungu kutoka Ulaya kuanzia karne ya 16, walikuwa wakiishi katika hali ya kimaumbile, ndipo ikaleta mlinganisho wa "waliostaarabika" na "wasiostaarabika." Kwa mujibu wa mkabala huu wa mawazo unaweza kuainisha nchi na mataifa katika yale yaliyostaarabika kuliko mengine au watu waliostaarabika kuliko wengine.

Milinganisho hii ilichangia kuzua nadharia ya Udarwin wa kijamii (Social Darwinism) ya Herhert Spencer na Maendeleo ya utamaduni (Cultural evolution) ya Lewis Henry Morgan. Jinsi baadhi ya wakosoaji wanavyosema, kutofautisha tamaduni za juu na za chini kwa kweli ni usemi wa mgogoro kati ya wasomi wa Ulaya na wasio wasomi, na kutofautisha watu wastaarabu na wasio wastaarabu kwa kweli ni usemi wa mgogoro kati ya madola ya kikoloni ya Ulaya na watawaliwa wao.

 
Mwanaanthropolojia wa Kiingereza kwa jina Edward Taylor ndiye aliyekuwa mtaalamu wa kwanza wa asili ya Uingereza kutumia neno utamaduni kwa usawa na kwa ubia.

Wahakiki wengine wa karne ya 19, wakifuata mfano wa Rosseau, wamekubali huu mgawiko wa utamaduni wa juu na wa chini; hata hivyo wameuona ubora na uchangamano wa utamaduni wa juu unaochugua na kuharibu hali halisi ya kimaumbile ya watu. Wahakiki hao walitilia mkazo muziki wa asili (jinsi unavyotolewa na watu wanaofanya kazi) uliotumiwa kuelezea hali halisi ya maisha kwa upande mwingine muziki wa zamani si wa halisi na umejaa uoza. Maoni hayo yaliwadhihirisha watu wa kiasilia kama washenzi na wasiostaarabika wanaoishi maisha halisi, ambayo si changamano, hayajabanangwa na mifumo ya kitabaka ya kiubepari ya kimagharibi.

Mnamo mwaka 1870 Edward Taylor (1832-1917) aliyatumia mawazo haya ya utamaduni wa juu na wa chini kupendekeza nadharia ya ukuaji wa dini. Kulingana na nadharia hiyo, dini hukua kutoka mfumo wa kuabudu miungu hadi ibada ya Mungu mmoja.[12] Aliielezea dini kama jumla ya shughuli zinazozitambulisha jamii za kibinadamu. Maoni hayo huchangia pakubwa kuelewa dhana ya utamaduni kwa sasa.</ref>

Dhana za karne ya 20

hariri

Ingawa wanaanthropolojia ulimwenguni huurejelea ufafanuzi wa Taylor, katika karne ya 20 dhana ya utamaduni ilijitokeza kama mhimili wa Anthropolojia ya Kimarekani, ambapo utamaduni ulifafanuliwa kama uwezo wa kiubia wa binadamu wa kuainisha na kusimbika tajiriba zao kiishara na kuwasilisha kiishara tajiriba zilizosimbikwa kijamii.

Anthropolojia ya Kimarekani imepangiliwa katika mawanda manne. Kila mojawapo huchangia sana utafiti wa utamaduni. Mawanda yenyewe ni: anthropolojia ya kibiolojia, isimu, anthropolojia ya kiutamaduni, na akiolojia. Utafiti katika mawanda haya umewaathiri kwa kiwango fulani wanaathropolojia wanaofanya kazi katika nchi zingine.

Elimu jamii

hariri

Sosholojia ya utamaduni inajihusisha na utamaduni unavyojitokeza katika jamii, nao unaweza ama kutegemea ama kutotegemea mata (yaani majengo, vifaa n.k. ama tunu, imani, taratibu n.k.).[13] t.

Kutokana na athari ya watu kama Karl Marx, Emile Durkheim na Max Weber, aina hii ya sosholojia ilitokea kwanza Ujerumani (19181933), ambapo wataalamu kama Alfred Weber walitunga neno Kultursoziologie (kwa Kiingereza cultural sociology), halafu katika nchi za lugha ya Kiingereza, hasa miaka ya 1960.

Mafunzo ya kiutamaduni

hariri

Nchini Uingereza, wanasosholojia na wasomi wengine walioathiriwa na Umarx, kama vile Stuart Hall na Raymond Williams, walianzisha mafunzo ya kitamaduni. Wakifuata nyayo za Walimbwende wa karne ya 19 walihusisha utamaduni na matumizi ya bidhaa na mambo ya ziada (kama vile sanaa, muziki, filamu, chakula, michezo na mavazi). Hata hivyo walielewa mitindo ya kula na ya anasa inaamuliwa na mahusiano ya uzalishaji ambayo iliwafanya kuangazia zaidi mahusiano ya kitabaka na mpangilio wa uzalishaji.[14][15] Nchini Marekani mafunzo ya kitamaduni yaliangazia pakubwa juu ya uchunguzi wa utamaduni pendwa yaani maana ya kijamii ya uzalishaji kwa wingi wa bidhaa za matumizi na anasa. Dhana hii ilibuniwa na Richard Hggart mnamo mwaka wa 1964 alipoanzisha mjini Birmingham Kituo cha mafunzo ya kisasa ya kitamaduni.(Centre for Contemporary Cultural Studies/CCCS).Tokea hapo kituo hicho kimehusishwa sana na Stuart Hall ambaye alichukua mahali pa Hoggart kama mkurugenzi.

Kuanzia miaka ya 1970 na kuendelea, kazi aliyoasisi Stuart Hall pamoja na wenzake Paul Wills, Dick Hebdige, Tony Jefferson na Angela McRobbie, waliunda muungano wa kiusomi wa kimataifa. Uwanja huu ulipokua kuungana mawanda mengine kama vile siasa ya kiuchumi,mawasiliano,sosholojia,nadharia ya kijamii,nadharia ya kifasihi,nadharia ya vyombo vya habari,mafunzo ya filamu/video,anthropolojia ya kitamaduni,falsafa,mafunzo ya makavazi, na sanaa ya historia ili kuchunguza matukio ya kitamaduni au matini za kitamaduni. Katika uwanja huu watafiti wanajikita juu ya namna tukio fulani linavyohusiana na masuala ya itikadi, utaifa, ukabila, tabaka la kijamii, na/au jinsia. Mafunzo ya kitamaduni yanahusisha maana na matendo ya kila siku ya maisha. Matendo haya yanahusisha namna watu wanavyofanya vitu fulani( kama vile kutazama runinga, au kula) katika utamaduni fulani. Uwanja huu huchunguza maana na matumizi watu huwekea vifaa na matendo fulani. Hivi karibuni ,vile ubepari umeenea kote duniani(mchakato uitwao utandawazi),mafunzo ya kitamaduni yameanza kuchanganua njia za kienyeji na za kilimwengu za kupinga kutawaliwa na Magharibi.

Katika muktadha wa mafunzo ya kitamaduni,wazo la matini halihusishi tu lugha iliyoandikwa bali huhusisha filamu,picha,fesheni, au mitindo ya nywele:matini za mafunzo ya kitamaduni hujumuisha sanaa-baki za maana za utamaduni. Vilevile uwanja huu hupanua dhana ya "utamaduni". "Utamaduni" kwa mtafiti wa mafunzo ya kitamaduni hujumuisha utamaduni asilia wa juu( utamaduni wa makundi tawala ya jamii)[16] na utamaduni pendwa na maana na matendo ya kila siku. Mawili ya mwisho ndiyo yanayotiliwa maanani na mafunzo ya kitamaduni. Mwelekeo zaidi na sasa ni mafunzo ya utamaduni linganishi unaotokana na uwanja wa fasihi linganishi na mafunzo ya kitamaduni.

Wasomi nchini Uingereza na Marekani walibuni aina tofauti za mafunzo ya kitamaduni baada ya kuasisiwa kwa taaluma hii miaka ya mwishoni mwa 1970. Aina ya mafunzo ya kitamaduni ya Uingereza yalianzishwa miaka ya 1950 na 1960 kutokana na athari ya kwanza Richard Hoggart,E.P.Thompson na Raymond Williams na baadaye Stuart Hall na wengineo katika kituo cha mafunzo ya kisasa ya utamaduni katika chuo kikuu cha Birmingham. Hii ilihusisha maoni ya kisiasa ya mrengu wa kushoto na shutuma dhidi ya utamaduni pendwa kuwa ulikuwa utamaduni wa umati wa kibepari. Ilijumuisha baadhi ya mawazo ya tahakiki ya Shule ya Frankfurt ya kiwanda cha utamaduni.(yaani utamaduni wa umati). Hii inajitokeza katika maandishi ya wasomi wa mwanzoni wa Uingereza wa mafunzo ya kitamaduni na athari zao: tazama (kwa mfano) kazi za Raymond Williams, Stuart Hall, Paul Willis na Paul Gilroy.

Nako nchini Marekani Lindlof na Taylor wanasema ya kwamba mafunzo ya kitamaduni yalikitwa katika utamaduni wa kiprigmatiki wa uliberali wa wingi".[17] Aina ya mafunzo ya utamaduni ya Marekani mwanzoni yalijihusisha zaidi na kuelewa namna hadhira ingechukulia matumizi ya utamaduni wa umati.Kwa mfano wakereketwa wa mafunzo ya utamaduni Marekani waliandika kuhusu vipengele vya kiliberali vya fandom. Tofauti baina ya mitazamo ya Marekani na Uingereza sasa imefifia. Watafiti wengine hasa katika mafunzo ya mwanzoni ya utamaduni Uingereza wanatumia ruwaza za kimarx katika taaluma hii. Huu mtindo wa kufikiria una athari kutoka kwa Shule ya Frankfurt,lakini athari kubwa inatoka kwa umarx muundo wa Louis Althusser na wengineo. Mkazo wa umarx asili ni juu ya maana ya uzalishaji . Ruwaza hii huchukua uzalishaji kwa wingi na hutambua uwezo/mamlaka huwa miongoni mwa wale wanaotoa sanaa baki. Katika mtazamo wa kimarx,wale wanaothibiti njia za uzalishaji (msingi wa uchumi) kimsingi ndiyo hutawala utamaduni. Mielekeo mingine kuhusu mafunzo ya utamaduni kama vile mafunzo ya ufeministi ya utamaduni,na maendeleo ya kimarekani katika taaluma yanajitenga na wazo hili. Wanashutumu umarx kwa maana moja ya utamaduni ambayo inaaminiwa na wote. Mielekeo isiyo ya umarx inapendekeza njia mbalimbali za kushughulikia utamaduni wa sanaa-baki huathiri maana ya zao. Wazo hili linaelezewa vizuri katika kitabu cha Paul du Gay na wengine, Doing Cultural Studies: The case of Sony Walkman, ambacho kinapinga wazo kwamba wale wanaozalisha bidhaa huthibiti maana ambazo watu huhusisha nazo. Mchanganuzi wa kifeministi wa utamaduni, mwananadharia na mwanahistoria wa sanaa Griselda Pollock alichangia katika mafunzo ya utamaduni akitumia mitazamo ya sanaa historia,saikolojiachanganuzi. Mwandishi Julia Kristeva ana ushawishi mkubwa akichangia kwa mafunzo ya kitamaduni kupitia taaluma za sanaa na saikolojia changanuzi ya ufeministi wa Kifaransa.

Mabadiliko ya kitamaduni

hariri
 
Picha ya karne ya 19 inayoonyesha wakazi wa Australia wakipinga kuwasili kwa Kapteni James Cook mwaka 1770

Uvumbuzi wa utamaduni unaamanisha uvumbuzi wowote mpya na unaopatikana kuwa wa manufaa kwa kikundi cha watu na unaelezewa katika tabia zao lakini haupo kama kitu kinachoonekana. Watu wako katika ulimwengu unaoharakisha mabadiliko ya utamaduni kiwakati,wakisukumwa na kupanuka kwa biashara kimataifa,vyombo vya habari,na kuongezeka kwa idadi ya watu miongoni mwa mambo mengine.

Tamaduni zinaathiriwa na nguvu zinazoleta mabadiliko na zile zinazopinga mabadiliko. Nguvu hizi zina uhusiano na miundo ya kijamii na matukio halisi na zinajihusisha katika kuendeleza mawazo na matendo ya kitamaduni ndani ya miundo ya sasa ambayo nayo inabadilika[18]. (Tazama umuundo.)

Mizozo ya kijamii na maendeleo ya kiteknolojia yanaweza kusababisha mabadiliko katika jamii kwa kubadili mikikimikiki ya kijamii kwa kukuza ruwaza mpya za utamaduni kwa kuwezesha tukio zalishi. Hii mihamisho ya kijamii huweza kuandamana na mihamisho ya kiitkadi na aina nyingine za mabadiliko ya kitamaduni. Kwa mfano muungano wa kifeministi wa Kimarekani ulihusisha matendo mapya yaliyosababisha uhamisho katika mahusiano ya kijinsia,kubadilisha jinsia na miundo ya kiuchumi. Hali ya kimazingira inaweza kuchangia. Mabadiliko huhusisha kufuata nguli wa kienyeji katika filamu. Kwa mfano,misitu ya kitropika ilirejea tena mwishoni mwa enzi ya theluji.mimea iliyofaa kwa kufugwa ilikuwepo,ikasababisha kuvumbuliwa kwa kilimo,ambacho kilisababisha uvumbuzi wa kitamaduni na mihamisho ya mikikimikiki ya kijamii[19].

 
Picha kamili ya mwanamke wa Turkman,akisimama kwenye zulia katika mlango wa yurt,akiwa amevalia nguo za kitamaduni pamoja na virembesho

Tamaduni huathirika kutoka nje kupitia kwa mwingiliano baina ya jamii,ambazo pia zinaweza kutoa—au kuzuia---mihamisho ya kijamii na mabadiliko katika matendo ya kitamaduni. Vita au ushindani juu ya rasilimali unaweza kuathiri maendeleo ya kiteknolojia na mikikimikiki ya kijamii. Kuongezea,mawazo ya kitamaduni yanaweza kuhama kutoka jamii moja hadi nyingine kupitia kwa kuenea na kwa mabadiliko ya uigaji wa utamaduni Fulani. Katika kuenea hali ya kitu(siyo lazima maana yake) hutoka utamaduni mmoja hadi mwingine. Kwa mfano,hamburgers ambazo ni za kawaida Marekani,zilionekana kuwa ngeni zilipoanzishwa Uchina. "Kuenea kunakoacha athari” (kubadilishana mawazo) hurejelea elementi za utamaduni mmoja kusababisha kuwepo kwa uvumbuzi au kusambazwa.kwa mwingine. "Ukopaji wa moja kwa moja” kwa upande mwingine hurejelea kuenea kwa kiteknolojia au kuenea kunakoonekana kutoka utamaduni mmoja hadi mwingine. Nadharia ya kuenea kwa uvumbuzi huwasilisha ruwaza ya utafiti ya kwa nini na lini watu na tamaduni huasilisha mawazo mapya,matendo na bidhaa.

Kuiga utamaduni fulani kuna maana tofauti lakini katika muktadha huu hurejelea kubadilishwa kwa tabia Fulani za utamaduni na utamaduni mwingine.Haya yamefanyika kwa makabila fulani ya Amerika na kwa makundi asilia ya watu kote ulimwenguni enzi za ukoloni. Michakato ya karibu kwa kiwango cha binadamu inahusisha usilimisho (binadamu kuasilisha utamaduni fulani) na kuwa na tamaduni nyingi.

Tanbihi

hariri
  1. "Meaning of "culture"". Cambridge English Dictionary. Iliwekwa mnamo Julai 26, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. James, Paul; with Magee, Liam; Scerri, Andy; Steger, Manfred B. (2015). Urban Sustainability in Theory and Practice: Circles of Sustainability. London: Routledge. uk. 53.
  3. Macionis, Gerber, John, Linda (2010). Sociology 7th Canadian Ed. Toronto, Ontario: Pearson Canada Inc. uk. 53.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  4. Harper, Douglas (2001). Online Etymology Dictionary
  5. Kroeber, AL na C. Kluckhohn, 1952. Culture: A Critical Review wa Concepts na Definitions.
  6. Immanuel Kant 1974 "Kujibu Swali: Ni nini Kutaalamika?" (Kwa Kijerumani: "Beantwortung der Frage: Was ist Aufklärung?") Berlinische Monatsschrift, Desemba (Berlin Monthly)
  7. Michael Eldridge, "The Kijerumani Bildung Mapokeo" UNC Charlotte Archived 23 Januari 2009 at the Wayback Machine.
  8. "Adolf Bastian", Sayansi Leo katika Historia; "Adolf Bastian", Encyclopaedia Britannica
  9. 9.0 9.1 Arnold, Mathayo. 1869. Utamaduni na Anarchy. Archived 6 Januari 2017 at the Wayback Machine.
  10. Williams (1983), p.90. Cited katika Shuker, Roy (1994). Kuelewa Popular Music, p.5. ISBN 0-415-10723-7. anasema kwamba kisasa fasili ya utamaduni kuanguka katika uwezekano tatu au mchanganyiko wa tatu zifuatazo:
    • "mchakato jumla ya kiakili, kiroho, na estetiska maendeleo"
    • "njia fulani ya maisha, kama ya watu, muda, au kundi"
    • "matendo na mazoea ya kitaaluma na hasa shughuli kisanaa".
  11. Bakhtin 1981, p.4
  12. McClenon, p.528-529
  13. Macionis, J., and Gerber, L. (2010). Sociology, 7th edition
  14. jina = "Williams"> Raymond Williams (1976) Keywords: A Vocabulary of Culture and Society Rev Ed. (Newyork: Oxford UP, 1983), uk. 87-93 na 236-8.
  15. Yohana Berger, Peter Smith Pub. Inc, (1971) Njia za Ukiangalia
  16. Bakhtin, Mikhail 1981. The Dialogic Imagination. Austin, TX: UT Press, p.4
  17. (Lindlof & Taylor, 2002, p.60
  18. O'Neil, D. 2006. "Mchakato wa Change". Archived 27 Oktoba 2016 at the Wayback Machine.
  19. Pringle, H. 1998. The Slow kuzaliwa ya Kilimo. Archived 1 Januari 2011 at the Wayback Machine. Sayansi 282: 1446.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri