Nyumba ya Mambo Msiige

Nyumba ya Mambo Msiige ni jengo la kihistoria kwenye ufukwe wa Shangani, Mji Mkongwe Zanzibar. Lilijengwa mnamo 1850 na tajiri mkazi wa Kiarabu, Salum bin Harith.[1][2]

Nyumba ya Mambo Msiige ikionekana kwa mbali.

Jengo hilo lilitumika kama makazi ya wawakilishi wa Waingereza, misheni ya Vyuo Vikuu katika Afrika ya kati na hospitali ya Uropa.[2]

Usanifu wa jengo lenyewe umejumuisha mchanganyiko wa kuvutia wa ushawishi wa Waswahili, Waajemi pamoja na matao ya mtindo wa Omani na uchoraji wa mbao.[3]

Marejeo hariri