Makazi (ekolojia)

(Elekezwa kutoka Makazi)

Makazi (kwa Kiingereza na Kilatini: habitat) kwa maana ya elimu ya ekolojia ni eneo au mazingira ambayo ni makao ya mnyama au mmea fulani au aina nyingine ya viumbe hai. Ni mazingira ya asili ambapo kiumbe huishi, au mazingira ambayo yanazunguka idadi ya jamii.

Makazi yaliyobaki ya Tembo wa Afrika
Ramani ya usambazaji inayoonyesha makazi mbalimbali ya kuzaa ya gali wenye mgongo mweusi

Ufafanuzi

hariri

Neno "idadi" huhusishwa na "kiumbe" kwa sababu, inawezekana kuelezea mazingira ya dubu mweusi mmoja, hatuna uwezo wa kutafuta dubu fulani au mmoja lakini kambi ya muungano wa dubu wakati wa kuzaa amabao huwa mahali fulani. Pia, makao hayo huweza kuwa tofauti na makao mengine ya kundi tofauti la dubu weusi. Hivyo, si jamii wala binafsi ambapo jina makazi kutumika.

Makazi madogo

hariri

Makazi madogo ni eneo ambalo ni nyumbani mwa viumbe wadogo sana, kama vile chaa wa mbao. Makazi madogo ni makazi ndani ya makazi makubwa, kwa mfano, kuni katika mti ulioanguka. Wadudu huishi kwenye makazi madogo, lakini kipande cha mti kinaweza kuwa makazi madogo kwani nyoka wanaweza kuishi ndani yake. Mazingira madogo ni eneo linalozunguka na masuala ya mmea binafsi au mnyama ndani ya makazi yake.

Makazi ya binadamu

hariri
Makala kuu: Makazi ya binadamu

Makazi ya binadamu ni mazingira ambayo binadamu huishi na kuingiliana.

Kwa mfano, nyumba ni makazi ya binadamu, ambapo binadamu hulala na kula.

Aina zake

hariri

Kuna makazi ya mjini na makazi ya vijijini.

Makazi ya mjini ni aina ya makazi ambayo watu wanajenga nyumba zao mijini, karibu na wenzao wengi.

Makazi ya vijijini ni aina ya makazi ambayo watu hujenga nyumba zao sehemu za vijijini.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Makazi (ekolojia) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.