Nyutoni (pia: newton) ni kizio cha kupima kazi.

Nyutoni moja

Fomula yake ni 1N = 1kg x m/s².


Maelezo yake ni nyutoni moja ni sawa na kani ikitumiwa kwa masi ya kilogramu 1 ikisogezwa kwa mchapuko wa mita 1 kwa sekunde.

Kwa lugha nyingine: Nyutoni 1 ni kani inayohitajika kuharakisha gimba linalolala kufika kasi ya katika kipindi cha sekunde moja.

Nyutoni ni kipimo cha SI. Jina linetokana na mwanafizikia Isaac Newton aliyegundua misingi ya fizikia umekanika.

1 N inalingana na kani ya uvutano wa dunia kwenye gimba dogo lenye masi ya gramu 102 kwenye uwiano wa bahari. Yaani mtu akishika tofah kando la bahari anatumia kani ya nyutoni moja.