Isaac Newton (25 Desemba 164220 Machi 1727) alikuwa mwanahisabati, mwanafizikia na mwanateolojia kutoka nchi ya Uingereza.

Isaac Newton mwaka 1689.
Kitabu chake Principia Mathematica, 1686.

Anakumbukwa duniani kote kutokana na michango yake mbalimbali katika sayansi.

Ndiye aliyegundua tawi la kalkulasi (sambamba na Leibniz), kanuni za mwendo na ya uvutano.

Mchango mwingine wa Isaac Newton upo katika nadharia ya nuru, akitumia mche kuonyesha jinsi rangi zinazounda nuru (kama zinavyoonekana kwenye upinde wa mvua) zinavyotokea.

Alichangia pia elimuanga kwa kuboresha darubiniakisi iliyoleta matokeo mazuri. Alitambua ya kwamba kanuni za uvutano zinatawala pia mwendo wa sayari. Alitunga ramani ya nyota kufuatana na tafiti za Flamsteed.

Elimu na imani

Newton alipata shahada yake ya kwanza mwaka 1665 na ile ya uzamili mwaka 1668.

Kwa kuwa alizaliwa katika familia ya Kianglikana, alitumia muda mwingi kufanya utafiti wa Biblia na theolojia pia. Alilenga kupatanisha elimu ya sayansi na imani yake. Aliandika "Uvutano unaeleza miendo ya sayari lakini haiwezi kueleza ni nani aliyeanzisha miendo yake. Mungu anatawala mambo yote na yaliyopo na yanayoweza kuwepo".

Tarehe 10 Desemba 1682 alimuandikia Richard Bentley: "Siamini ulimwengu unaweza kuelezwa na sababu za maumbile tu, bali nalazimika kuuona kama tunda la hekima na ubunifu vya mmoja mwenye akili". Hata hivyo, yeye binafsi hakukubali mafundisho juu ya Utatu wa Mungu.

Maandishi yake

Marejeo

  • Ball, W.W. Rouse (1908). A Short Account of the History of Mathematics. New York: Dover. ISBN 978-0-486-20630-1. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Christianson, Gale (1984). In the Presence of the Creator: Isaac Newton & His Times. New York: Free Press. ISBN 978-0-02-905190-0. This well documented work provides, in particular, valuable information regarding Newton's knowledge of Patristics
  • Craig, John (1958). "Isaac Newton – Crime Investigator". Nature. 182 (4629): 149–52. Bibcode:1958Natur.182..149C. doi:10.1038/182149a0.
  • Craig, John (1963). "Isaac Newton and the Counterfeiters". Notes and Records of the Royal Society of London. 18 (2): 136–45. doi:10.1098/rsnr.1963.0017.
  • Levenson, Thomas (2010). Newton and the Counterfeiter: The Unknown Detective Career of the World's Greatest Scientist. Mariner Books. ISBN 978-0-547-33604-6.
  • Manuel, Frank E (1968). A Portrait of Isaac Newton. Belknap Press of Harvard University, Cambridge, MA. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Stewart, James (2009). Calculus: Concepts and Contexts. Cengage Learning. ISBN 978-0-495-55742-5. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Westfall, Richard S. (1980). Never at Rest. Cambridge University Press. ISBN 978-0-521-27435-7. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Westfall, Richard S. (2007). Isaac Newton. Cambridge University Press. ISBN 978-0-19-921355-9. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Westfall, Richard S. (1994). The Life of Isaac Newton. Cambridge University Press. ISBN 978-0-521-47737-6. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • White, Michael (1997). Isaac Newton: The Last Sorcerer. Fourth Estate Limited. ISBN 978-1-85702-416-6. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)

Marejeo mengine

Dini

  • Dobbs, Betty Jo Tetter. The Janus Faces of Genius: The Role of Alchemy in Newton's Thought. (1991), links the alchemy to Arianism
  • Force, James E., and Richard H. Popkin, eds. Newton and Religion: Context, Nature, and Influence. (1999), pp. xvii, 325; 13 papers by scholars using newly opened manuscripts
  • Pfizenmaier, Thomas C. (Januari 1997). "Was Isaac Newton an Arian?". Journal of the History of Ideas. 58 (1): 57–80. Bibcode:1961JHI....22..215C. doi:10.1353/jhi.1997.0001. JSTOR 3653988.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Ramati, Ayval. "The Hidden Truth of Creation: Newton's Method of Fluxions" British Journal for the History of Science 34: 417–38. in JSTOR, argues that his calculus had a theological basis
  • Snobelen, Stephen "'God of Gods, and Lord of Lords': The Theology of Isaac Newton's General Scholium to the Principia", Osiris 2nd series, Vol. 16, (2001), pp. 169–208 in JSTOR
  • Snobelen, Stephen D. (1999). "Isaac Newton, Heretic: The Strategies of a Nicodemite". British Journal for the History of Science. 32 (4): 381–419. doi:10.1017/S0007087499003751. JSTOR 4027945.
  • Wiles, Maurice. Archetypal Heresy. Arianism through the Centuries. (1996) 214 pages, with chapter 4 on eighteenth century England; pp. 77–93 on Newton, excerpt and text search.

Viungo vya nje

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Isaac Newton kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.