Kani (kwa Kiingereza force) ni athira ya nje inayoweza kubadilisha hali ya utulivu au mwendo kwenye gimba. Hupimwa kwa nyutoni.[1]

Kani huelezwa pia kama nguvu ya kuvuta au kusukuma gimba lolote; mifano ya chanzo cha kani ni graviti au usumaku

Kani huwa na tabia za kiwango (ukubwa) na mwelekeo. Alama yake ni F.

Dhana ya kani iliundwa na Isaac Newton. Alisema katika kanuni yake ya pili kuwa :. Hapo ni kani,
ni masi ya gimba,
na ni mchapuko wa gimba.

Fomula inasema ya kwamba kama kani iko juu ya gimba litakuwa na mwendo na mwendo huo utaongezeka zaidi na zaidi.

Kama kani ni dhaifu na masi ya gimba ni kubwa itachukua muda mwingi hadi gimba litapata mchapuko mkubwa. Lakini kama kani ni kubwa na masi ya gimba ndogo litakimbia haraka karibuni sana.

Marejeo hariri

  1. KAST 1995, uk. 105

Viungo vya Nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.