Nzi-matunda
Nzi wa maembe (Bactrocera dorsalis)
Nzi wa maembe (Bactrocera dorsalis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Diptera (Wadudu wenye mabawa mawili tu)
Nusuoda: Brachycera (Diptera wenye vipapasio vifupi)
Familia ya juu: Tephritoidea
Familia: Tephritidae
Newman, 1834
Ngazi za chini

Nusufamilia 6:

Nzi-matunda ni nzi wa familia Tephritidae katika oda Diptera wanaoshambulia matunda duniani kote. Mabuu yao huishi ndani ya matunda mbalimbali yakiiva mitini ambamo wanajilisha na nyama ya matunda hayo. Nzi wa familia Drosophilidae huitwa nzi-matunda pia, lakini hawa ni wadogo zaidi na hula matunda yanayooza kwa kawaida. Ni bora kuwaita nzi-matunda wadogo.

Nzi-matunda ni wadogo kuliko nzi-nyumbani na spishi nyingi zina rangi kali na mabawa yenye mabaka meusi, kahawia au njano. Kichwa ni kifupi na kwa umbo la tufe nusu. Paji ni pana. Mabuu ni weupe, njano au kahawia.

Majike huingiza mayai yao katika matunda au sehemu nyingine za mimea na miti. Baada ya kutoka kwenye mayai mabuu huanza kujilisha na tishu ambamo hujikuta. Kwa sababu kunaweza kuwa mabuu mengi katika tunda moja, wanaweza kuletea wakulima hasara nyingi. K.m. nzi wa maembe anaharibu maembe mengi bila hatua za kuwadhibiti.

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashriki hariri

Picha hariri