Mdudu Mabawa-mawili

(Elekezwa kutoka Diptera)
Mdudu mabawa-mawili
Nzi-mweleaji (Mesembrius insignis)
Nzi-mweleaji (Mesembrius insignis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Diptera (Wadudu wenye mabawa mawili tu)
Ngazi za chini

Nusuoda 2:

Wadudu mabawa-mawili ni wadudu wadogo wa oda Diptera (di = mbili, ptera = mabawa) ambao wana mabawa mawili tu. Wadudu wengine wana mabawa manne au hawana mabawa, isipokuwa wadudu mabawa-potwa walio na mabawa mawili pia.

Spishi zenye vipapasio virefu kwa umbo wa uzi huitwa mbu au kisubi na zinaainishwa katika nusuoda Nematocera. Spishi zenye vipapasio vifupi huitwa nzi na zinaainishwa katika nusuoda Brachycera.

Spishi za mbu zinazojulikana sana ni spishi za anofelesi (Anopheles spp.) na za kuleksi (Culex spp.) ambazo hufyunza damu na kurithisha magonjwa. Spishi za nzi zinazojulikana sana ni nzi wa nyumba (Musca domestica) na nzi buluu (Calliphora vomitoria).

Spishi kadhaa za Afrika

hariri

Nematocera:

Brachycera:

  Makala hiyo kuhusu "Mdudu Mabawa-mawili" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.