Omar Brown
Omar Brown (alizaliwa 21 Juni 1982 katika mji wa Trelawny) ni mwanariadha wa nchi ya Jamaika ambaye ni mtaalam katika mbio ya 200m.
Yeye alikuwa na mafanikio mengi akiwa mwanariadha kijana huku akishinda medali ya fedha na shaba katika mbio za 200m na 100m katika Mashindano ya Mabingwa vijana wa Dunia katika mwaka wa 1999. Mwaka uliofuata alichukua nafasi ya nne katika Mashindano ya Mabingwa Vijana wa Dunia. Aliwakilisha Chuo Kikuu cha Arkansas katika mashindano kati ya vyuo vikuu.
ALishinda mbio ya mita 200 katika Michezo ya Jumuia ya Madola ya 2006, akaorodheshwa kama nambari tisa duniani katika mbio ya mita 200 katika mwaka huo na gazeti la Track and Field News.
Katika mwaka wa 2007, yeye alimwoa mwanariadha wa Olimpiki wa Jamaika, Veronica Campbell. Yeye alipata jeraha mwaka huo kwenye kifudio. Alirudi kushiriki katika mbio za majaribio za Jamaika za 2008 lakini akapata jeraha jingine mguuni kutokana na kukimbia katika mtindo tofauti.Alikimbia kwa njia tofauti kwa kuwa alikuwa na maumivu kwenye kifudio. Alifanyiwa upasuaji mnamo Septemba 2008 kurekebisha shida fulani lakini kovu tishu iliyobaki ilimzuia kurudi kushiriki katika mbio. Hakurudi hadi mwisho wa msimu wa 2009 alipochukua nafasi ya nne katika mbio ya mita 200 katika Shindano la Shanghai Golden Grand Prix.
Ubora wa binafsi
haririTukio | Muda (sekunde) | Pahali pa kushindana | Tarehe |
---|---|---|---|
Mbio ya mita 60 | 6.72 | Lexington, Kentucky, Marekani | 28 Februari 2004 |
Mbio ya mita 100 | 10.27 | Kingston, Jamaika | 21 Julai 2000 |
Mbio ya mita 200 | 20.33 | Carson, California, Marekani | 21 Mei 2006 |
Mbio ya mita 400 | 46.00 | Walnut, California, Marekani | 17 Aprili 2005 |
- Habari hii imetolewa kutoka wasifu katika IAAF
Marejeo
hariri- Williams, Gordon (2009-01-20). Sprinter takes it slow - Omar Brown coming back from injury layoff Archived 6 Agosti 2012 at the Wayback Machine.. The Jamaica Star.
- Campbell-Brown, Veronica (2009-10-07). Veronica Campbell Brown named Unesco Ambassador - IAAF Online Diaries Archived 12 Januari 2010 at the Wayback Machine.. IAAF.
- Shanghai Golden Grand Prix Results. ESPN (2009-09-20).
Viungo vya nje
hariri- IAAF wasifu wa Omar Brown